Ndege ya kwanza kati ya Israel na UAE yaondoka Tel Aviv, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 31, 2020 at 1:00 pm

August 31, 2020

 Ndege ya kwanza ya moja kwa moja kati ya Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE imeondoka leo asubuhi, takriban wiki tatu baada ya nchi hizo mbili kusaini mkataba wa kihistoria wa diplomasia. Ndege hiyo ya shirika la ndege la Israel, El Al imeondoka kwenye uwanja wa ndege wa Tel Aviv wa Ben Gurion kuelekea Abu Dhabi. Ndege hiyo Boeing 737-900 imeandikwa neno ”amani” kwa Kiarabu, Kiingereza na Kiebrania, juu ya dirisha la rubani. Tal Becker, rubani wa ndege hiyo amewaambia waandishi habari kwamba hiyo ni safari ya kusisimua katika maisha yake na hisia maalum. Abiria wa ndege hiyo ni pamoja na ujumbe mkubwa wa Waisraeli, mshauri wa serikali ya Marekani, Jared Kushner na washauri wa usalama wa Marekani na Israel, Robert O’Brien na Meir Ben-Shabbat, miongoni mwa wengine.,

 

Ndege ya kwanza ya moja kwa moja kati ya Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE imeondoka leo asubuhi, takriban wiki tatu baada ya nchi hizo mbili kusaini mkataba wa kihistoria wa diplomasia.

 Ndege hiyo ya shirika la ndege la Israel, El Al imeondoka kwenye uwanja wa ndege wa Tel Aviv wa Ben Gurion kuelekea Abu Dhabi. 

Ndege hiyo Boeing 737-900 imeandikwa neno ”amani” kwa Kiarabu, Kiingereza na Kiebrania, juu ya dirisha la rubani. 

Tal Becker, rubani wa ndege hiyo amewaambia waandishi habari kwamba hiyo ni safari ya kusisimua katika maisha yake na hisia maalum. 

Abiria wa ndege hiyo ni pamoja na ujumbe mkubwa wa Waisraeli, mshauri wa serikali ya Marekani, Jared Kushner na washauri wa usalama wa Marekani na Israel, Robert O’Brien na Meir Ben-Shabbat, miongoni mwa wengine.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *