Nchi za Magharibi zaitaka Urusi kujieleza kuhusu Navalny,

October 2, 2020

Mataifa matano wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yameitaka Urusi kujieleza juu ya kupewa sumu kwa mkosoaji mkuu wa serikali ya nchi hiyo Alexei Navalny, hali waliyoileza kuwa ni “tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.” 

Barua iliyoandikwa jana na Ujerumani, Uingereza, Ubelgiji, Estonia na Ufaransa, imewasilishwa katika baraza hilo usiku wa kuamkia leo ambapo Urusi inachukua urais wa jopo hilo kwa mwezi wa Oktoba. 

Hapo jana Navalny alimshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa kuamuru kumpa sumu. Alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya barua hiyo, Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia aliomba ushirikiano kutoka katika nchi za Ulaya.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *