Nchi za Baltic kumuwekea vikwazo Lukashenko, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 31, 2020 at 1:00 pm

August 31, 2020

Rais wa Lithuania, Gitanas Nauseda amesema nchi za Baltic zitatangaza vikwazo vya kusafiri kwa maafisa wapatao 30 wa Belarus, akiwemo Rais Alexander Lukashenko. Rais Nauseda amewaambia waandishi habari kwamba vikwazo hivyo vitawekwa baadae leo na nchi za Lithuania, Latvia na Estonia. Hata hiyo, amesema idadi hiyo ni hatua ya kwanza na inaweza ikaongezeka baadaye. Awali, Lithuania ilisema inakusudia kuwawekea vikwazo maafisa wa Belarus wanaohusika na kukiuka sheria za uchaguzi na kuwakandamiza waandamanaji.Wakati huo huo, kiongozi wa upinzani wa Belarus, Sviatlana Tsikhanouskaya anatarajiwa kulihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Ijumaa ijayo. Msemaji wake amesema Sviatlana atazungumza kwa njia ya video, baada ya kualikwa na Estonia, ambayo kwa sasa ni mjumbe asiye wa kudumu wa baraza hilo. Sviatlana aligombea uchaguzi wa urais wa Agosti 10 nchini Belarus, ambao wafuasi wake wanasema alishinda.,

Rais wa Lithuania, Gitanas Nauseda amesema nchi za Baltic zitatangaza vikwazo vya kusafiri kwa maafisa wapatao 30 wa Belarus, akiwemo Rais Alexander Lukashenko. 

Rais Nauseda amewaambia waandishi habari kwamba vikwazo hivyo vitawekwa baadae leo na nchi za Lithuania, Latvia na Estonia. 

Hata hiyo, amesema idadi hiyo ni hatua ya kwanza na inaweza ikaongezeka baadaye. Awali, Lithuania ilisema inakusudia kuwawekea vikwazo maafisa wa Belarus wanaohusika na kukiuka sheria za uchaguzi na kuwakandamiza waandamanaji.

Wakati huo huo, kiongozi wa upinzani wa Belarus, Sviatlana Tsikhanouskaya anatarajiwa kulihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Ijumaa ijayo. 

Msemaji wake amesema Sviatlana atazungumza kwa njia ya video, baada ya kualikwa na Estonia, ambayo kwa sasa ni mjumbe asiye wa kudumu wa baraza hilo. 

Sviatlana aligombea uchaguzi wa urais wa Agosti 10 nchini Belarus, ambao wafuasi wake wanasema alishinda.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *