Nchi tano za Ulaya zalaani hatua ya Israel ya ujenzi Ukingo wa Magharibi,

October 16, 2020

 

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Ufaransa, Uhispania, Italia na Uingereza leo wameikosoa hatua ya Israel kujenga maelfu ya nyumba mpya za makaazi katika eneo la Wapalestina inalolikalia kimabavu kwenye Ukingo wa Magharibi. 

Katika taarifa ya pamoja wizara hizo zimesema kuwa hatua hiyo inakiuka sheria ya kimataifa na kuondoa zaidi uwezekano wa kupatikana suluhu la mataifa mawili kwa ajili ya kupatikana haki na amani ya kudumu katika mzozo huo wa Palestina na Israel. 

Shirika la kutetea haki za binadamu la Peace Now linasema Baraza Kuu la Mipango la Israel hapo juzi na jana liliidhinisha ujenzi wa karibu nyumba elfu 5 katika eneo hilo. 

Nchi hizo tano zimetoa wito wa kusitishwa mara moja kwa ujenzi huo na pia kuondolewa kwa nguvu kwa Wapalestina na kuvunjwa kwa nyumba zao Jerusalem Mashariki na Ukingo wa Magharibi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *