Nchi 1O wanachama wa EU kuwachukua watoto 400 kutoka kambi ya Moria, on September 11, 2020 at 1:00 pm

September 11, 2020

Maelfu ya waomba hifadhi wamelala nje kwa usiku wa tatu kwenye kisiwa cha Lesbos baada ya kambi kubwa kabisa ya wahamiaji nchini Ugiriki kuteketea kwa moto. Polisi wamefika kwa wingi leo katika eneo hilo huku wengine wakiwazuia wahamiaji kufika katika bandari iliyo karibu. Maafisa wa Ugiriki wamewalaumu wahamiaji kwa tukio hilo la moto katika kambi ya Moria, ambalo lilitokea baada ya watu 35 kupatikana na virusi vya corona na walikuwa chini ya vizuizi. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya ndani wa Ujerumani Horst Seehorfer amesema nchi 10 wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekubali kuwachukua karibu watoto wadogo 400 wasioandamana na mtu kutoka kambi hiyo iliyoungua. Ujerumani na Ufaransa zitachukua idadi kubwa ya watoto hao, kila nchi ikijitolea kuwachukua 100 hadi 150.,

Maelfu ya waomba hifadhi wamelala nje kwa usiku wa tatu kwenye kisiwa cha Lesbos baada ya kambi kubwa kabisa ya wahamiaji nchini Ugiriki kuteketea kwa moto.

 Polisi wamefika kwa wingi leo katika eneo hilo huku wengine wakiwazuia wahamiaji kufika katika bandari iliyo karibu. 

Maafisa wa Ugiriki wamewalaumu wahamiaji kwa tukio hilo la moto katika kambi ya Moria, ambalo lilitokea baada ya watu 35 kupatikana na virusi vya corona na walikuwa chini ya vizuizi. 

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya ndani wa Ujerumani Horst Seehorfer amesema nchi 10 wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekubali kuwachukua karibu watoto wadogo 400 wasioandamana na mtu kutoka kambi hiyo iliyoungua. 

Ujerumani na Ufaransa zitachukua idadi kubwa ya watoto hao, kila nchi ikijitolea kuwachukua 100 hadi 150.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *