NATO yapongeza kuanza kwa mazungumzo ya amani ya Afghanistan nchini Qatar, on September 12, 2020 at 4:00 pm

September 12, 2020

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jenerali Jens Stoltenberg leo hii ameipongeza hatua ya kuanza mazungumzo kati ya Taliban na serikali ya Afghanistan kwa kusema ni “fursa ya kihistoria.” Katika ukurasa wake wa Twitter ameandika “Naukaribisha mwanzo wa mazungumzo ya amani ya Waafghanistan leo,” aidha aliendelea kutoa ahadi kwamba NATO itasimama pamoja na raia wa Afghanistan katika kuilinda hatua hiyo na kuhakikisha taifa hilo kamwe halitarejea tena kuwa hifadhi ya magaidi. Mazungumzo hayo yanayoungwa mkono na Marekani yameanza mapema leo nchini Qatar, pamoja na kwamba bado vurugu zinaendelea kuligubika taifa la Afghanistan.,

 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jenerali Jens Stoltenberg leo hii ameipongeza hatua ya kuanza mazungumzo kati ya Taliban na serikali ya Afghanistan kwa kusema ni “fursa ya kihistoria.” 

Katika ukurasa wake wa Twitter ameandika “Naukaribisha mwanzo wa mazungumzo ya amani ya Waafghanistan leo,” aidha aliendelea kutoa ahadi kwamba NATO itasimama pamoja na raia wa Afghanistan katika kuilinda hatua hiyo na kuhakikisha taifa hilo kamwe halitarejea tena kuwa hifadhi ya magaidi. 

Mazungumzo hayo yanayoungwa mkono na Marekani yameanza mapema leo nchini Qatar, pamoja na kwamba bado vurugu zinaendelea kuligubika taifa la Afghanistan.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *