NATO kuimarisha vikosi vya usalama Iraq, on September 17, 2020 at 6:00 pm

September 17, 2020

 Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema muungano huo umeazimia kuimarisha vikosi vya usalama vya Iraq.Kulingana na taarifa iliyotolewa na NATO, Katibu Mkuu Jens Stoltenberg na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Hüseyin wamekutana katika makao makuu ya NATO huko Brussels, Ubelgiji.Staltenberg amesema katika mkutano huo kwamba NATO na Iraq zinaendelea kufanya kazi kwa karibu katika mapambano dhidi ya ugaidi, na akasema kuwa vikosi vya usalama vya Iraq vinavyopambana dhidi ya Daesh vimejitoa muhanga kwa kiasi kikubwa.Stoltenberg amesisitiza kujitolea kwa NATO kusaidia kuimarishwa kwa vikosi vya usalama vya Iraq.NATO ilikubali kuanzishwa kwa kikosi cha NATO Iraq mnamo Oktoba 2018, kwa ombi la serikali ya Iraq, bila ya kuwa na nia ya kupigana, bali kwa lengo la mafunzo na kujenga uwezo.Mawaziri wa Ulinzi wa NATO walifanya uamuzi mnamo Februari wa kuendeleza kazi zao nchini Iraq.,

 Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema muungano huo umeazimia kuimarisha vikosi vya usalama vya Iraq.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na NATO, Katibu Mkuu Jens Stoltenberg na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Hüseyin wamekutana katika makao makuu ya NATO huko Brussels, Ubelgiji.

Staltenberg amesema katika mkutano huo kwamba NATO na Iraq zinaendelea kufanya kazi kwa karibu katika mapambano dhidi ya ugaidi, na akasema kuwa vikosi vya usalama vya Iraq vinavyopambana dhidi ya Daesh vimejitoa muhanga kwa kiasi kikubwa.

Stoltenberg amesisitiza kujitolea kwa NATO kusaidia kuimarishwa kwa vikosi vya usalama vya Iraq.

NATO ilikubali kuanzishwa kwa kikosi cha NATO Iraq mnamo Oktoba 2018, kwa ombi la serikali ya Iraq, bila ya kuwa na nia ya kupigana, bali kwa lengo la mafunzo na kujenga uwezo.

Mawaziri wa Ulinzi wa NATO walifanya uamuzi mnamo Februari wa kuendeleza kazi zao nchini Iraq.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *