Naombeni Ushauri Kila Nikifanya Mapenzi Bila Zana Napata Ujauzito

October 19, 2020

Mimi ni Msichana wa Miaka 25 , Tatizo langu ni kuwa kila nikifanya mapenzi na mvulana bila kutumia zana lazima nipate mimba, nilianza kuwajua wanaume toka nikiwa na miaka 21 siku niliyotolewa bikira nilipata mimba pia ikanibidi niitoe kwa vile nilikuwa nasoma ..sasa kuanzia kipindi hicho nikifanya tu lazima nipate mimba nimeshatoa mimba kumi na tano mpaka sasa, Nimejaribu kufuata Calender lakini wapi…Je hili ni Tatizo ama nimelogwa ? Nimekuwa mtu wa kufanya abortion kila wakati mpaka naogopa sasa nisije haribu kizazi changu nikashindwa kuzaa muda muafaka wa kuwa na mtoto………………..

Help pliz

Mimi Mdau ..Msinitukane jamani

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *