Nani wa kulaumiwa kwa usambaaji wa magonjwa ya kusataajabisha?

October 18, 2020

Dakika 10 zilizopita

Short-nosed fruit bat, Thailand

Mara nyingi Dkt. Mathieu Bourgarel huwa anatafuta ruhusa kutoka kwa wazee wa kijiji kwenda kutembelea mapango ambayo matambiko huwa yanafanyika huko.

Akiwa amevalia barakoa, na nguo za kujikinga mpaka mikononi, aliingia mapangoni ambako kuna giza, alitumia kamba kushuka mpaka chini ya mapango.

Harufu ya Popo iko kila mahali na uchafu wao ukiwa chini ya sakafu.

Mara nyingine, Popo akitoka kulala huwa anakung’uta mabawa yake wakati anapotaka kuruka.

Watu kutoka sehemu ya Zimbabwe wanawaita popo, panya wanaoruka ambao ni waovu.

Kama ilivyo maeneo mengine duniani, wanyama wanaoruka wamekuwa hawaeleweki.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa wanyama pori anasema wanyama hao ni viumbe wazuri.

“Wanavutia,” amesema. “Watu wanaogopa kitu ambacho hawakifahamu.”

Dkt. Bourgarel ambaye ni muwindaji wa virusi kutoka taasisi ya utafiti nchini Ufaransa, Cirad, anafanyakazi na walimu wa chuo kikuu cha Zimbabwe ya kukusanya sampuli katika mapango.

Cave, Zimbabwe

Utafiti ni sehemu ya juhudi za uchunguzi wa kimataifa wa vinasaba na mengine mengi kuhusu virusi vinavyosambazwa na popo na kuvumbua mbinu zinazoweza kutumika kwa haraka ikiwa watu wataaanza kuwa wagonjwa.

“Watu wa eneo mara nyingi hutembelea makazi ya Popo hao ili kutafuta kinyesi chake na kukitumia kama mbolea kwa mazao yao. Hivyobasi ni muhimu kujua pathojeni zinazobebwa na popo kwasababu zinaweza kusambazwa hadi kwa wanadamu,” amesema daktari Elizabeth Gori wa chuo kikuu cha Zimbabwe.

Wanasayansi wanakadiria kwamba magonjwa mapya matatu kati ya manne yakuambukiza kwa mwanadamu chanzo chake ni wanyama.

Onyo la hatari hiyo lilitolewa mwaka 2002, wakati magonjwa ya ajabu kama vile Sars yalipoanza kujitokeza nchini China na kusababisha vifo vya watu karibu 800 kote dunani.

Mwaka 2017, watafiti walibaini popo wanaoishi katika mapango mkoa wa Yunnan waliokuwa na chembe za vinasaba vya virusi vya Sars vilivyo kwa binadamu.

Wakati huo walionya kwamba kuna uwezekano wa kutokea kwa ugonjwa sawa na huo tena na hilo likatokea.

Going into the cave

Lakini badala ya kulaumu spishi moja au nyingine, kinachohitajika kufanyika ni kutathmini tena uhusiano wetu na dunia asilia, amesema daktari Rocha kuwa Popo ni muhimu kwa mfumo wa ikolojia na ustawi wa mwanadamu.

Lakini kuanza kulenga au kumaliza wanyama wanaoruka juu ya mazao.

Mimea ya maeneo ya kitropiki hutegemea wanyama kama Popo kwa uchavushaji ikiwemo kakao, vanila na matunda ya duriani.

Na husambaza mbegu za mimea zinazopatikana katika maeneo ya misitu yanayopokea mvua kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Bats, Mexico
Maelezo ya picha,

Popo wajitokeza kutoka kwa pango lenye mawe ya chokaa huko Mexico

Itakuwa jambo la kusikitisha ikiwa Popo wataanza kuogopewa kwasababu kusambaa kwa magonjwa kutoka kwa wayama hadi kwa mwanadamu kunahusiana zaidi na mwanadamu kuingilia makazi ya wanyama, amesema daktari David Robertson wa chuo kikuu cha Glasgow.

Bila shaka vinavyohusika katika usambaaji wa ugonjwa wa Sars-CoV-2 vimekuwa vikisambaa kwa popo kwa miongo mingi na kuna uwezekano wa kusambaza maambukizi kwa spishi zingine za wanyama pia.

Kumekuwa na taarifa kadhaa zinazoangazia kutaka kudhuru popo kunakohusishwa na ugonjwa wa Covid-19 ikiwemo kudhamiria kuwaua huko Peru, India, Australia, China na Indonesia.

Egyptian fruit bat
Maelezo ya picha,

Baadhi ya popo kutoka maeneo ya kitropiki hubeba mbegu na kuzisambaza maeneo ya mbali mno

Wanasayansi wanaonya kwamba hatua kidogo tu zisizofaa huenda zikasababisha athari kubwa kwa makundi ya wanyama walio katika hatari ya kupotea na hata kuongeza hatari ya ugonjwa huo kuongezeka.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Virusi vya corona: Popo wamekuwa wakilaumiwa kwa kueneza virusi

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *