Naibu wa rais wa Kenya apasua mbarika baada ya kuzuiliwa kwenda Uganda

August 4, 2021

Naibu wa Rais wa Kenya Wiliam Ruto hatimaye amezungumzia kisa cha Jumatatu ambapo alizuiliwa kusafiri nchi jirani ya Uganda kwa ziara ya kibinafsi .

Katika mahojiano na kituo cha Radio cha Inooro kinachomilikiwa na Kampuni ya Royal Media, Bwana Ruto alisema kufutwa kwa safari yake ni hatua ya kumdunisha akisimulia changamoto alizopitia yeye na washirika wake.

”Tuna shida. Wabunge wengi wamefukuzwa katika kamati za bunge. Nimewekwa pembeni. Kwa hivyo, kile kilichofanyika (katika Uwanja wa Ndege wa Wilson) ilikuwa hatua ya kunidhalilisha na kunifanya nionekane sina maana”, alisema.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *