Mzozo wa Syria: Marekani yapeleka vikosi zaidi baada ya kuzozana na Urusi

September 19, 2020

Dakika 8 zilizopita

Gari la kijeshi la Marekani likishika doroa katika uwanhja mmoja nchini Syria

Maelezo ya picha,

Mamia kadhaa ya wanajeshi wa Marekani wamesalia katika kaskazini mashariki mwa Syria

Marekani imeongeza idadi ya wanajeshi wake Syria baada ya malumbano kati yake na Urusi kuzua hali ya taharuki nchini humo.

Maafisa wa Marekani wanesema magari sita ya vita na karibu wanajeshi 100 wamepelekwa kaskazini mashariki mwa Syria.

Visa vya makabiliano kati ya vikosi vya Marekani na Urusi vinavyoweka ulinzi katika nchi hiyo vimeongezeka mwaka huu.

Kapteni wa jeshi la majni la Marekani Bill Urban amesema hatua hiyo itasaidia “kuhakikisha usalama wa vikosi vya muungano”.

Ameongeza kuwa, pamoja na magari hayo ya vita amabyo yalikuwa Kuwait, Marekani pia itapeleka “Vifaa vya ulizi wa angani” na kuongeza “doria za mara kwa mara ya doria zinazofanywa dhidi ya vikosi hivyo”.

“Marekani haina mpago wa kuzozana na nchi nyingine Syria, lakini italinda vikosi vya muungano ikilazimika kufanya hivyo,” Bwana Urban, ambaye ni msemaji wa majeshi ya Marekani alisema, katika taarifa siku ya Ijumaa.

Bwana Urban hakutaja Urusi kwa jina, lakini katika taarifa nyingine kutoka kwa maafisa wa Marekani, iliyoangaziwa kwanza na kituo cha habari cha NBC, aliashiria anazungumzia nchi hiyo.

“Hatua hii inatuma “ishara kwa Urusi” kujiepusha na vitendo vya “uchokozi” kaskazini mashariki mwa Syria,” alisema afisa mmoja ambaye jina lake halikutajwa.

Kituo cha NBC kiliwanukuu maafisa hao wakidaiwa kusema kwamba wanajeshi zaidi na magari ya kivita yamepelekwa kaskazini mashariki mwa Syria ili kuzuia vikosi vya Urusi kuingia katika maeneo ya usalama ambako vikosi vya Muungano vya Marekani vikosi vya Kikurdi vinaendesha oparesheni.

Kwa miaka kadhaa sasa, kumeshuhudiwa mzozo wa mara kwa mara kati ya vikozi vya Marekani na Urusi nchini Syria. Lakini matukio ya wiki za hivi karibuni kaskazini mashariki mwa Syria vimeongeza uhasama kati ya nchi hizo mbili.

Mwisho wa mwezi Agosti, wanajeshi saba wa Marekani walijeruhiwa baada ya gari lao kugonhgana na gari la kijeshi la Urusi. Serikali za Urusi na Marekani zililaumiana kufuatia tukio hilo ambalo lilinaswa kwenye kanda ya video na kuwekwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Video hiyo inaonesha gari la kijeshi la Urusi katika msafara wa jangwani ukigongana na gari la kijeshi la Marekani, Helikopta ya Urusi ilipaa umbali wa chini kabisa.

Urusi inasema kuwa Marekani ilizuia doria.

Marekani ilisema Urusi iliingia katika ”eneo la usalama” ambalo walikuwa wamekubali hawatafika.

Urusi kwa upande wake inasema kuwa ilitoa taarifa mapema kwamba vikosi vyake vitafanya oparesheni katika eneo hilo

Transparent line
Screenshot from video clip of collision (Rusvesna.su/youtube)

Maelezo ya picha,

Picha inayoonesha makabiliano hayo iliwekwa kwenye tuvuti ya Urusi ya Rusvesna.su

Marekani ina karibu wanajeshi 500 katika eneo hilo – ambao ni wachache ikilinganishwa na idadi ya awali iliyokuwa hapo- kusaidia kuweka ulinzi na kuvunja tishio lolote kutoka kwa wanamgambo wa kijihadi wa kundi la Islamic State.

Uchambuzi na maswala ya ulinzi Jonathan Marcus

Kumekuwa na matukio kadhaa yanayohusisha wanajeshi wa Marekani kaskazini mwa Syria. Wiki kama moja hivi iliyopita ilikuwa na makabiliano makali na Urusi, washirika wa Syria.

Februari 2018, kundi kumbwa la mamluki la jeshi la Urusi lilizindua mashambulio dhidi ya eneo la Marekani karibu na eneo kubwa la mafuta na wanajeshi wake wakapata majeraha.

Ingawa tukio hilo la hivi karibuni ni tofauti kidogo. Chanzo chake ni makabiliano ya moja kwa moja kati ya maafisa wa jeshi wa Urusi na vikosi vya Marekani. Marekani inasisitiza kwamba hilo ni sehemu ya matukio ambayo yamekuwa yakitokea. Urusi inakiuka makubaliano ya eneo.

Kwanini hilo limetokea? Urusi inaiona Marekani kama inayokaribia kuondoka Syria. Oktoba mwaka jana, Rais wa Marekani Donald Trump aliamua kuondoa wanajeshi 1,000 ambao walikuwa wakiunga mkono muungano wa Kikurdi, lakini akabadilisha mawazo yake na kubakisha wanajeshi kidogo katika eneo ambalo limewekewa masharti mengi.

Lakini Urusi inafahamu kwamba Bwana Trump anataka kupunguza wanajeshi wa Marekani nje ya nchi. Na vilevile, inaonekana kutaka sana Marekani ijiondoe.

Source link

,Dakika 8 zilizopita Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Mamia kadhaa ya wanajeshi wa Marekani wamesalia katika kaskazini…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *