Mzozo mto Nile: Marekani kukata fungu la msaada kwa Ethiopia, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 3, 2020 at 10:00 am

September 3, 2020

Marekani inaripotiwa kwamba imepunguza msaada wa Ethiopia wa dola milioni 100 kutokana na utata wa bwawa kubwa la uzalishaji umeme linalojengwa kutoka kwa kijito cha mto Nile.Vyazo vya serikali vimesema kwamba hilo limechochewa na hatua ya Ethiopia ya kuanza kujenga bwawa kabla ya kufikia makubaliano na Misri na Sudan.Ehtiopia imesema kwamba inataka bwawa hilo kwa mradi wa upatikanaji wa umeme.Bwawa hilo likishamalizwa kujengwa, litakuwa kubwa zaidi katika uzalishaji wa umeme Afrika na kutoa huduma za umeme kwa hadi raia milioni 65 wa Ethiopia.”Karibu dola milioni 100 hivi zitaathirika, ambapo dola milioni 26 ni ufadhili unaomalizika mwisho wa mwaka wa fedha,” chanzo cha bunge la Marekani kimezungumza na shirika la habari la Reuters.Ufadhili unaoathirika unahusishwa na lishe bora, usalama wa eneo na mipaka, ushindani wa kisiasa na ujenzi, afisa amesema. Ufadhili wa miradi inayohusishwa na ugonjwa wa ukimwi, uhamiaji, usaidizi kwa wakimbizi na mpango wa amani wa chakula pia utaathirika.Afisa kutoka idara ya Marekani ameliambia shirika la Reuters kwamba uamuzi wa Ethiopia wa kaunza kujaza bwawa hilo wakati majadiliano na Misri na Sudan yanaendelea yameshusha uaminifu uliokuwepo kwenye mazungumzo na pia kumeathiria nia ya kujitolea kwa Ethiopia.”Awali, Marekani ilionesha wasiwasi wake mara kadhaa kwamba kuanza kujaza bwawa hilo kabla ya hatua zote za kiusalama kuchukuliwa kunaongeza uwezekano wa kutokea kwa hatari kubwa,” afisa huyo alisema.Kilimo cha nchini Ethiopia kinategemea maji ya mto NileCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESBalozi wa Ethiopia nchini Marekani ameliambia gazeti la Financial Times kuwa ni matumaini yake Marekani itabadili msimamo kuhusu punguzo hilo.”Tumewaomba kufikiria tena uamuzi wao tunasubiri. Ni matumaini yetu kwamba uhusiano wa kidplomasia wa miaka 117 hautaathirika kwasababu ya suala ambalo halina uhusiano wowote na nchi hizi mbili,” Fitsum Arega amesema.Wanahabari wanasema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa inaweza kuonekana kama hatua ya Rais Donald Trump kuishinikiza Ethiopia baada ya nchi hiyo kukataa mazungumzo na Misri na Sudan.Chanzo cha bwawa kubwa la Gerd ni kijito cha mto kilichopo Misri na lina uwezo wa kudhibiti kiwango cha maji kwa nchi hiyo. Mto Nile ndio chanzo kikuu cha maji ya kunywa na kilimo kwa Misri.,

Marekani inaripotiwa kwamba imepunguza msaada wa Ethiopia wa dola milioni 100 kutokana na utata wa bwawa kubwa la uzalishaji umeme linalojengwa kutoka kwa kijito cha mto Nile.

Vyazo vya serikali vimesema kwamba hilo limechochewa na hatua ya Ethiopia ya kuanza kujenga bwawa kabla ya kufikia makubaliano na Misri na Sudan.

Ehtiopia imesema kwamba inataka bwawa hilo kwa mradi wa upatikanaji wa umeme.

Bwawa hilo likishamalizwa kujengwa, litakuwa kubwa zaidi katika uzalishaji wa umeme Afrika na kutoa huduma za umeme kwa hadi raia milioni 65 wa Ethiopia.

“Karibu dola milioni 100 hivi zitaathirika, ambapo dola milioni 26 ni ufadhili unaomalizika mwisho wa mwaka wa fedha,” chanzo cha bunge la Marekani kimezungumza na shirika la habari la Reuters.

Ufadhili unaoathirika unahusishwa na lishe bora, usalama wa eneo na mipaka, ushindani wa kisiasa na ujenzi, afisa amesema. Ufadhili wa miradi inayohusishwa na ugonjwa wa ukimwi, uhamiaji, usaidizi kwa wakimbizi na mpango wa amani wa chakula pia utaathirika.

Afisa kutoka idara ya Marekani ameliambia shirika la Reuters kwamba uamuzi wa Ethiopia wa kaunza kujaza bwawa hilo wakati majadiliano na Misri na Sudan yanaendelea yameshusha uaminifu uliokuwepo kwenye mazungumzo na pia kumeathiria nia ya kujitolea kwa Ethiopia.

“Awali, Marekani ilionesha wasiwasi wake mara kadhaa kwamba kuanza kujaza bwawa hilo kabla ya hatua zote za kiusalama kuchukuliwa kunaongeza uwezekano wa kutokea kwa hatari kubwa,” afisa huyo alisema.

Kilimo cha nchini Ethiopia kinategemea maji ya mto NileCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Balozi wa Ethiopia nchini Marekani ameliambia gazeti la Financial Times kuwa ni matumaini yake Marekani itabadili msimamo kuhusu punguzo hilo.

“Tumewaomba kufikiria tena uamuzi wao tunasubiri. Ni matumaini yetu kwamba uhusiano wa kidplomasia wa miaka 117 hautaathirika kwasababu ya suala ambalo halina uhusiano wowote na nchi hizi mbili,” Fitsum Arega amesema.

Wanahabari wanasema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa inaweza kuonekana kama hatua ya Rais Donald Trump kuishinikiza Ethiopia baada ya nchi hiyo kukataa mazungumzo na Misri na Sudan.

Chanzo cha bwawa kubwa la Gerd ni kijito cha mto kilichopo Misri na lina uwezo wa kudhibiti kiwango cha maji kwa nchi hiyo. Mto Nile ndio chanzo kikuu cha maji ya kunywa na kilimo kwa Misri.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *