Mzee wa Utopolo awapa onyo kali Manara na Manula, noreply@blogger.com (Udaku Special)

August 30, 2020

Mzee wa Utopolo awapa onyo kali Manara na ManulaHizi ni tambo za wiki ya Wananchi wa Klabu ya Yanga ambayo inakamilishwa leo kwa kutambulisha wachezaji wapya, jezi mpya na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya nchini Burundi kuanzia 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Benjamin William Mkapa. Kamera za EATV & EA Radio Digital imempata shabiki kindakindaki wa timu hiyo Mzee wa Utopolo ambaye amefunguka matarajio ya timu yake, pia amempa onyo kipa wa Simba Aishi Manula na msemaji wa timu hiyo Haji Manara juu ya uwezo wa mchezaji wao mpya Carlinhos. “Historia ya mchezaji wetu Carlinhos inavyosemekana makipa wengi waliokuwa wanajaribu kufuata mipira yake wameishia Hospitali, ukijaribu kufuata mipira yake mikononi basi ujue viganja hauna, namuonya sana Aishi Manula akijaribu kufuata mipira ya huyu bwana basi ni Hospitali moja kwa moja” amesema Mzee wa Utopolo Akizungumzia onyo lake kwa Haji Manara Mzee wa Utopolo ameongeza kusema “Ujumbe wangu kwa Manara namuomba jumapili akae kwenye station ashuhudie wananchi tunavyofaana, pia nampa onyo maana anavyoongea abakize maneno kwa sababu Oktoba hatuchezi Simba na Yanga tunacheza timu ya babu na wajukuu” ,

Mzee wa Utopolo awapa onyo kali Manara na Manula

Hizi ni tambo za wiki ya Wananchi wa Klabu ya Yanga ambayo inakamilishwa leo kwa kutambulisha wachezaji wapya, jezi mpya na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya nchini Burundi kuanzia 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Benjamin William Mkapa. 

Kamera za EATV & EA Radio Digital imempata shabiki kindakindaki wa timu hiyo Mzee wa Utopolo ambaye amefunguka matarajio ya timu yake, pia amempa onyo kipa wa Simba Aishi Manula na msemaji wa timu hiyo Haji Manara juu ya uwezo wa mchezaji wao mpya Carlinhos. 

“Historia ya mchezaji wetu Carlinhos inavyosemekana makipa wengi waliokuwa wanajaribu kufuata mipira yake wameishia Hospitali, ukijaribu kufuata mipira yake mikononi basi ujue viganja hauna, namuonya sana Aishi Manula akijaribu kufuata mipira ya huyu bwana basi ni Hospitali moja kwa moja” amesema Mzee wa Utopolo 

Akizungumzia onyo lake kwa Haji Manara Mzee wa Utopolo ameongeza kusema “Ujumbe wangu kwa Manara namuomba jumapili akae kwenye station ashuhudie wananchi tunavyofaana, pia nampa onyo maana anavyoongea abakize maneno kwa sababu Oktoba hatuchezi Simba na Yanga tunacheza timu ya babu na wajukuu” 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *