Mwili wa mama yake P Funky kuzikwa Kilosa Morogoro, on September 10, 2020 at 10:00 am

September 10, 2020

 Familia ya mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, P Funk Majani imetangaza kifo cha mama yake mzazi Aunt Sheilah ambacho kimetokea Septemba 8, nchini Uholanzi wakati akipatiwa matibabu.Mipango ya Mazishi inaendelea kufanywa, kwa sasa Msiba upo Kilosa mkoani Morogoro na ndipo atazikiwa huko kwa sasa mipango ya kurudisha mwili  wa Mama P Funk Majani inaratibiwa. Kaka wa Marehemu Fadhili Kiholi amesema “Mpaka sasa hivi mwili bado upo Uholanzi pia tunafanya michakato ya mwili kurejea hapa nchini, tutaondoka leo jioni na taratibu zote tunatarajia kuzifanya wiki ijayo, Marehemu alikuwa akiishi Tanzania na alienda Uholanzia mwezi wa 9 mwaka jana kama sehemu ya matibabu, huwa anaendaga mara kwa mara Uholanzi ila muda huu amekaa kidogo, pia mipango ya mazishi itafanyika Kilosa Morogoro kwenye ardhi aliyozaliwa”.,

 

Familia ya mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, P Funk Majani imetangaza kifo cha mama yake mzazi Aunt Sheilah ambacho kimetokea Septemba 8, nchini Uholanzi wakati akipatiwa matibabu.

Mipango ya Mazishi inaendelea kufanywa, kwa sasa Msiba upo Kilosa mkoani Morogoro na ndipo atazikiwa huko kwa sasa mipango ya kurudisha mwili  wa Mama P Funk Majani inaratibiwa.

 Kaka wa Marehemu Fadhili Kiholi amesema “Mpaka sasa hivi mwili bado upo Uholanzi pia tunafanya michakato ya mwili kurejea hapa nchini, tutaondoka leo jioni na taratibu zote tunatarajia kuzifanya wiki ijayo, Marehemu alikuwa akiishi Tanzania na alienda Uholanzia mwezi wa 9 mwaka jana kama sehemu ya matibabu, huwa anaendaga mara kwa mara Uholanzi ila muda huu amekaa kidogo, pia mipango ya mazishi itafanyika Kilosa Morogoro kwenye ardhi aliyozaliwa”.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *