Mwarabu Fighter Afunguka Kumlinda Baba wa Rihanna

October 9, 2020

MOJA ya story zilizo-trend wiki hii ni ‘bodyguard’ maarufu Bongo aliyewahi kufanya kazi na Diamond Platnumz na wasanii wengine maarufu nchini, Mwarabu Fighter,  kupiga picha na baba mzazi wa msanii Rihanna Ronald Fenty ambaye amekuja kutembea hapa nchini Tanzania.

Inasemekana Mwarabu Fighter amepata dili la kumlinda baba huyo kipindi hiki ambacho yupo  nchini, ambapo amesema:

“Wale ni wageni tu, walikuja sehemu ambayo nilikuwepo ila hakuna jambo lolote, walivyoona mishe zangu wakajua ninachokifanya maana kuna mteja wangu nilikuwa namlinda, kwa hiyo wakasogea kwangu wakawa wananiuliza maswali na tukabadilishana baadhi ya vitu kwa nia ya kibiashara zaidi, yote yanatokea ni mipango ya Mungu,” alisema Mwarabu.

Akizungumzia kufanya kazi na msanii Alikiba baada ya kuonekana kwenye mchezo wa SamaKiba ‘Foundation’, Mwarabu amesema:

“Mimi nilisapoti SamaKiba kwa sababu ni kitu kikubwa wanachokifanya kwenye jamii hadi nikapiga naye picha ila sikupewa kazi ya kumlinda.,” amesema.

Aidha, amesema sasa hivi ana vijana ambao anawafundisha kuhusu kazi ya kuwalinda wasanii ambapo kama msanii atahitaji kufanya nao kazi atawatoa kwa makubaliano binafsi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *