Mwanaume wa India aliyeokolewa kutoka friji ya chumba cha kuhifadhia maiti afariki

October 17, 2020

Dakika 6 zilizopita

Salem freezer
Maelezo ya picha,

Bw Balasubramanyam aliwekwa ndani ya friji ya chumba cha kuhifadhia maiti baada ya kutangazwa kimakosa kuwa amekufa

Mwanaume wa India mwenye umri wa miaka 74, ambaye alitangazwa kuwa amekufa kimakosa na kuwekwa ndani ya friji katika jimbo la Tamil Nadu , amefariki dunia siku kadhaa baada ya kuokolewa.

Bw Balasubramanyam alitangazwa kuwa amekufa siku ya Jumatatubaada ya kupelekwa hospitalini. Haijabainika wazi ni tatizo gani alilolipata.

Aliwekwa ndani ya friji ya chumba cha kuhifadhia maito hadi kesho yake wakati ambapo wahudumu wa maiti walipokuja kuchukua mwili wakekwa ajili ya mazishi walipomuona akitikisika na kubaini kuwa kumbe alikuwa bado yungali hai.

Walimpeleka katika hospitali ya pili lakini baadaye alipoteza maisha Ijumaa.

Mkuu wa hospitali ya serikali katika mji wa kusini wa Salem, Dkt Balajinathan, amesema kuwa mgonjwa huyo alikuwa amelazwa akiwa katika hali dhaifu baada ya kuokolewa katikafriji ya maiti na kufa kutokana na matatizo ya mapafu.

Unaweza pia kusoma:

Aliiambia BBC mjini Tamil kuwa haijafahamika wazi ni masaa mangapi Bw alikuwa ndani ya friji ya kuhifadhia maiti.

Baada ya kutangazwa na daktari kuwa amekufa katika hospitali ya kibinafsi, familia yake ilichukua mwili wake nyumbani kwao , na kuwaita wachimba kaburi walete friji ya kuuhifadhia mwili wake.

Halafu wakawafahamisha ndugu , jamaa na marafiki kuwa watamzika siku ya Jumanne.

Kampuni ya mazishi ilisema waliambiwa kuwa kaka yake Balasubramanyam alikuwa “amesaini barua ya daktari juu ya kifo chake “.

Mkuu wa polisi wa Salem Senthil Kumar amesema kuwa familia imeshindwa kuonyesha cheti cha kimatibabu kinachoonesha kifo cha Balasubramanyam.

Wamewasilisha kesi dhidi ya familia yake kwa”kufanya ukatili au uzembe uliohatarisha maisha ya binadamu “.

Familia inadai kwamba pia alikuwa na matatizo ya neva, kulingana mkuu wa polisi.

Bw Balasubramanyam aliishi na mke wake, mabinti zake wawili na kaka yake.

Haijafahamika wazi ni vipi aliweza kuishi hai katika friji iliyokuwa na barafu ndani ya boksi- au iwapo hospitali ya kibinafsi ambako alitangazwa kuwa amekufa pia inachunguzwa.

BBC imejaribu kuwasiliana na hospitali hiyo ya kibinfsi na familia, lakini hakuna hata mmoja wao ambaye amekubali kuzungumzia tukio hilo na daktari aliyetangaza kifo chake hajatoa tamko lolote kuhusiana na Bw Balasubramanyam

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *