Mwanaume auza zawadi ya pombe alizopewa kusherehekea siku yake kuzaliwa kununua nyumba

September 7, 2020

Dakika 8 zilizopita

Matthew Robson alipatiwa chupa ya Whiskey yenye umri wa miaka 18 kila mwaka ili kusherehekea sikua yake ya kuzaliwa
Maelezo ya picha,

Matthew Robson alipatiwa chupa ya Whiskey yenye umri wa miaka 18 kila mwaka ili kusherehekea sikua yake ya kuzaliwa

Mwanaume mmoja ambaye baba yake alimpa zawadi ya pombe kwa miaka 18 kila ilipotimia siku ya yake ya kuzaliwa anaziuza ili kununu nyumba.

Matthew Robson, kutoka Taunton, alizaliwa mwaka 1992 na katika maisha ya baba yake Pete ametumia takriban pauni 5,000 kununua chupa 28 za pombe moja aina ya Macallan

Hadi sasa chupa hizo zina thamani ya pauni 40,000 na sasa zinauzwa.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 28 “huenda haikuwa ” zawadi nzuri kwa mvulana mdogo lakini kwa “maagizo ya kwamba asizifungue kamwe chupa hizo ” zimekua sawa na mayai katika kiota cha ndege.

Pete Robson alisema kwamba Whiskey hiyo haikua zawadi ya pekee , alimpatia mwanawe Mathew kama zawadi ya siku ya kuzaliwa kwake
Maelezo ya picha,

Pete Robson alisema kwamba Whiskey hiyo haikua zawadi ya pekee , alimpatia mwanawe Mathew kama zawadi ya siku ya kuzaliwa kwake

Matthew anasema kwamba alikuwa chini ya maagizo makali kutofungua pombe yake siku ya kuzaliwa kwake
Maelezo ya picha,

Matthew anasema kwamba alikuwa chini ya maagizo makali kutofungua pombe yake siku ya kuzaliwa kwake

“Kila mwaka nilipokea chupa moja kama zawadi ya kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa ,” Matthew alisema. “Nilidhani ni zawadi ndogo ya ajabu kwasababu nilikuwa mdogo sana kuanza kunywa.

“Lakini nilipewa masharti makali, nisiwahi hata siku moja kufungua na nilijaribu sana kujitahidi na nikafanikiwa na chupa zote bado zimefungwa.

Baba yake Pete, ambaye ni mkazi wa Milnathort in Scotland, alisema chupa ya kwanza ya whisky ya mwaka 1974 ilinunuliwa kwa ajili ya “kulewesha kichwa cha mtoto mchanga”.

“Nilifikiri litakua ni jambo la kufurahisha kama ningenunua chupa moja kila mwaka ili awe na machupa 18 atakapotimiza umri wa miaka 18 whisky ,” alisema.

“Haikuwa zawadi pekee aliotuletea. Ilikuwa tu ni zawadi ya kipekee, lakini ilikuwa ni bahati kidogo kwamba iliendelea .”

Pombe ya Whisky

Tangu wakati huo, wataalamu wanasema pombe hizo aina ya Macallan zimekusanywa na Matthew anatumaini kuziuza kwa pauni 40,000 na kutumia pesa hizo kununulia nyumba.

Inauzwa na mlanguzi wa whisky Mark Littler, ambaye alizielezea kama described it “pombe zinazofaa”.

“Thamani ya pombe ya Macallan imepanda sana katika kipindi cha miaka 5 hadi 10 .” Kuwa na kiwango cha aina hiyo cha chupa zake zitauzwa sana .”

Alisema kuwa “idadi kubwa ya watu ambao wameelezea utashi ” wa kuzinunua, hasa kutoka kwa wanunuzi mjini New York na bara la Asia.

Source link

,Dakika 8 zilizopita Maelezo ya picha, Matthew Robson alipatiwa chupa ya Whiskey yenye umri wa miaka 18 kila mwaka ili…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *