Mwanamke wa kwanza Marekani kukabiliwa na hukumu ya kifo ya serikali kuu tangu 1953

October 18, 2020

Dakika 8 zilizopita

Lisa Montgomery in jail

Maelezo ya picha,

Lisa Montgomery amepangiwa kukabiliana na hukumu ya kifo Desemba 8

Marekani inatekeleza hukumu ya kifo kwa mfungwa wa kike kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miaka 70, kulingana na Wizara ya Sheria.

Lisa Montgomery alimyonga mwanamke mjamzito huko Missouri kabla ya kumkata mama huyo tumbo lake na kumtoa mtoto aliyekuwa amembeba mwaka 2004.

Anatarajiwa kuchomwa au kudungwa sindano ya sumu Desemba 8.

Mwanamke wa mwisho kuhukumiwa kifo na serikali ya Marekani alikuwa Bonnie Heady, aliyekufariki dunia kwenye chumba cha gesi huko Missouri mwaka 1953, kulingana na kituo cha taarifa za adhabu ya kifo.

Hukumu ya serikali dhidi ya Brandon Bernard, ambaye pamoja na washirika wake waliwauwa mawaziri wawili vijana mwaka 1999, pia imepangiwa kutolewa Desemba.

Mwanasheria mkuu William Barr alisema uhalifu huo “ni vitendo vya kinyama”.

Mwaka jana, utawala wa Trump ulisema kuwa utaanza tena kutekeleza hukumu ya kifo.

Lisa Montgomery ni nani?

Desemba 2004, Montgomery alisafiri kutoka Kansas hadi nyumbani kwa Bobbie Jo Stinnett, huko Missouri, kwa madai kwamba ameenda kununua mbwa, kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Sheria.

“Wakiwa ndani ya makaazi, Montgomery alimshambulia na kumnyonga Bi. Stinnett – aliyekuwa na ujauzito wa miezi nane – hadi mwathirika akapoteza fahamu,” taarifa iliyotolewa inasema.

“Kwa kutumia kisu cha jikoni, Montgomery alikata tumbo la Bi. Stinnett kulikosababisha arejeshe fahamu. Wakaanza kukabiliana na Montgomery akamnyonga Stinnett hadi akafariki dunia. Kisha, Montgomery akamtoa mtoto aliyekuwa kwenye tumbo la Stinnett, na kumchukua mtoto huyo akijaribu kujifanya kuwa ni wake.”

Mwaka 2007, jopo lilimpata Montgomery na hatia ya kuteka nyara kulikosababisha kifo kulingana na sheria za serikali nchini Marekani, na kwa kauli moja wakapitisha hukumu ya kifo dhidi ya mtuhumiwa.

Hata hivyo wakili wa Montgomery wanasema ubongo wa mteja wake uliathirika kwasababu ya kichapo alichopigwa akiwa mtoto hivyobasi hayuko sawa kiakili na kutokana na hilo mteja wake hastahili kuhumiwa kifo.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya sauti,

Hukumu ya kifo kuanza tena Marekani

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *