Mwanamke mja mzito miongoni mwa watu sita waliouwawa na bomu huko Afghanistan,

October 16, 2020

 

Maafisa wanasema mwanamke mmoja mja mzito ni miongoni mwa watu sita waliouwawa baada ya gari lao kukanyaga bomu lililokuwa limetegwa pembezoni mwa barabara katika mkoa wa magharibi mwa Afghanistan wa Ghor. 

Abdul Maruf Ramesh ni msemaji wa polisi na ameliambia shirika la habari la Ujerumani,dpa kuwa watu hao walikuwa wanaelekea hospitali kwa kuwa ulikuwa muda wa kujifungua wa mwanamke huyo.

Maafisa wamelilaumu kundi la Taliban kwa tukio hilo wakisema mabomu hayo ya kutega barabarani ndiyo silaha yao wanayoipenda. Mabomu hayo hutegwa yakiwa na lengo la kushambulia misafara ya wanajeshi na maafisa wa serikali ila mara nyingi raia ndio wanaoishia kuwa wahanga.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *