Mwanamke aanguka kutoka kwa gari Uingereza akinasa video ya Snapchat

September 19, 2020

Dakika 3 zilizopita

M25

Maelezo ya picha,

Mwanamke huyo alianguka katika barabara kuu inayoelekea makutano ya M25 kuelekea mjini wa Westharm nchini Uingereza

Mwna mke mmoja ameanguka kutoka kwa gari katika barabara kuu ya kwenda Westharm,Uingereza baada ya mlango wa gari aliokuwa akitegemea kuchukua video ya Snapchat kufunguka.

Mwanamke huyo hakujeruhiwa vibaya lakini polisi wanasema “aliponea kifo”.

Alitibiwa katika eneo la tukio na wahudumu wa afya. Hakuna mtu aliyekamatwa, polisi walisema.

Katika ujumbe uliowekwa kwenye Twitter, polisi wakitengo cha usalama bara barani walisema: “Kiti cha abiria upande wa mbele kilikuwa kikining’inia nje ya gari wakati mwanamke huyo alipokuwa akichukua video ya Snapchat katika barabara ya M25. Baadae alianguka barabarani kutoka kwa gari hilo.

“Ana bahati sana hakujeruhiwa vibay aau kufariki. #nowords”

Tweet

Maelezo ya picha,

Afisa wa Surrey alielezea jinsi mwanamke huyo alivyonusurika kifo

Msemaji wa polisi katika eneo hilo alisema: “Maafisa waliitwa katika barabara kuu ya M25 mapema asubuhi kufuatia ripoti kwamba abiria ameanguka kutoka kwa gari lililokuwa likienda.

Source link

,Dakika 3 zilizopita Chanzo cha picha, Google Maelezo ya picha, Mwanamke huyo alianguka katika barabara kuu inayoelekea makutano ya M25…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *