Mwanaharakati wa Hong Kong akamatwa kwa maneno ya ”uchochezi”, on September 6, 2020 at 1:00 pm

September 6, 2020

Mwanaharakati mmoja wa upinzani mjini Hong Kong Tam Tak-chi, amekamatwa leo na kikosi kipya cha polisi kwa kutamka maneno ya uchochezi saa chache kabla ya mkutano wa hadhara dhidi ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa inayokabiliwa na utata.Kukamatwa kwa Tak-Chi, ni tukio la hivi karibuni la kuzuiliwa kwa wafuasi mashuhuri wanaounga mkono demokrasia katika eneo hilo na kumetokea siku ambayo raia mjini humo walitarajiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliocheleweshwa kutokana na janga la virusi vya corona.Kulingana na afisa mmoja mkuu wa polisi Li kwai-wah, Tam alikamatwa kutokana na maneno ya uchochezi chini ya Sheria ya Uhalifu sehemu ya kumi, akimaanisha sheria iliyotungwa katika enzi ya ukoloni wa Uingereza ili kubana matamshi dhidi ya serikali.Tangu sheria ya usalama wa kitaifa ilipopitishwa Beijing na kutekelezwa Hong Kong mnamo 30 Juni, watu 21, pamoja na mmilki wa chombo cha habari anayetetea demokrasia Jimmy Lai na mwanaharakati mashuhuri Agnes Chow, wamekamatwa kwa madai ya uchochezi wa kujitenga, kushirikiana na vikosi vya kigeni na vitendo vya ugaidi.,

Mwanaharakati mmoja wa upinzani mjini Hong Kong Tam Tak-chi, amekamatwa leo na kikosi kipya cha polisi kwa kutamka maneno ya uchochezi saa chache kabla ya mkutano wa hadhara dhidi ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa inayokabiliwa na utata.

Kukamatwa kwa Tak-Chi, ni tukio la hivi karibuni la kuzuiliwa kwa wafuasi mashuhuri wanaounga mkono demokrasia katika eneo hilo na kumetokea siku ambayo raia mjini humo walitarajiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliocheleweshwa kutokana na janga la virusi vya corona.

Kulingana na afisa mmoja mkuu wa polisi Li kwai-wah, Tam alikamatwa kutokana na maneno ya uchochezi chini ya Sheria ya Uhalifu sehemu ya kumi, akimaanisha sheria iliyotungwa katika enzi ya ukoloni wa Uingereza ili kubana matamshi dhidi ya serikali.

Tangu sheria ya usalama wa kitaifa ilipopitishwa Beijing na kutekelezwa Hong Kong mnamo 30 Juni, watu 21, pamoja na mmilki wa chombo cha habari anayetetea demokrasia Jimmy Lai na mwanaharakati mashuhuri Agnes Chow, wamekamatwa kwa madai ya uchochezi wa kujitenga, kushirikiana na vikosi vya kigeni na vitendo vya ugaidi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *