Mwakinyo kuzichapa Novemba 13, kuwania mataji mawili,

October 16, 2020

 

Bondia Hassan Mwakinyo atapanda ulingoni Novemba 13 kuzichapa kuwania mataji ya dunia ya WBF na wa mabara wa IBA.

Bondia huyo namba moja nchini kwenye uzani wa super welter atazichapa na Jose Carlos Paz wa Argentina pambano la raundi 12.

Pambano hilo limepewa jina  la ‘Dar Fight Night’ limeandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports na limepangwa kufanyika Next Door Arena, Masaki, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Jackson Group, Kelvin Twissa amesema pambano la #Mwakinyo litakuwa la kutetea ubingwa wa WBF wa dunia alioshinda dhidi ya Tshibangu Kayembe wa DRCongo.

Akizungumzia maandalizi yake, #Mwakinyo amesema yuko vizuri na amejipanga si tu kutetea ubingwa wa dunia, lakini pia kutwaa taji jingine la kimataifa.

Pia siku hiyo kutakuwa na pambano la kumsindikiza Mwakinyo na Paz, ambapo bondia Abdallah Pazi maarufu kwa jina la #DullahMbabe atazichapa na Alex Kabangu wa DR Congo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *