Mvua zaleta maafa makubwa Dar, watu 12 wafariki dunia,

October 15, 2020

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepokea taarifa ya vifo vya watu kumi na mbili vilivyotokana na athari ya mvua inayoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa Jumla ya watu 8 walifariki dunia baada ya kusombwa na maji mkoa wa kipolisi Ilala, huku mkoa wa kipolisi Kinondoni wakifariki watu wanne.

“Oktoba 13, 2020 kuanzia majira ya saa kumi alfajiri katika maeneo mbalimbali yaJ iji la  Dar es Salaam, mvua kubwa ilianza kunyesha na kuendelea kunyesha mchana kutwa na kusababisha vifo vya watu 12” Kamanda Mambosasa.

Aliendelea kusema “Katika mkoa wa kipolisi Ilala jumla ya watu 8 walifariki dunia baada ya kusombwa na maji akiwemo mwanamke mmoja aliyefahamika kwa majinaya Mariam Yahaya (45), Mkazi wa Vingunguti, alifariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akijaribu kuokoa vyombo vyake vilivyokuwa vinasombwa na maji ambapo mwili wake ulikutwa unaelea kando ya mto Msimbazi na mwili wamarehemu umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili”.

Aidha,miili ya watu watano ilipatikana katika bonde la mto Msimbazi eneo la Jangwani, kati yahao watu wawili walifahamika kwa majina kama ifuatavyo; Herieth Kanuti (18), Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Lutihinda na Ipyana Mwakifuna (19)  Mkazi wa Jangwani, Askari Jeshi la akiba la Mgambo na miili mingine ya watu watatu bado haijatambuliwa ikiwa ni wanaume wawili na mwanamke mmoja.

“Tukio lingine la kifo limeripotiwa leo Oktoba, 14,2020 majira ya saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano asubuhi huko Tabata, mwili wa mtu mmoja mwanaume aliyefahamika kwa majina ya Philipo  Feliciani 30), Mkazi wa Tabata Kimanga, ulionekana ukiwa umenasa kwenye matope katika mtoTenge, ambaye alifariki dunia Oktoba 13,2020 majira ya saa kumi na mbili jioni baada ya kudondoka na kusombwa na maji alipojaribu kuvuka kwenye kidaraja cha waenda kwa miguu kilichopo Tabata Kimanga na mwili wa mtu mmoja mwingine mwanaume asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka  30-35 alikutwa akiwa amefariki dunia katika eneo la Ukonga sabasaba mji mpya” alisema Mambosasa. 

Pia katika mkoa wa kipolisi Kinondoni Jumla ya watoto wawili wafamilia moja na watu wazima wawili walifariki dunia kutokana na athari zamvua ambaoni:-

1. IbrahimHassani(24),MkaziwaKigogoBuyuni,

2. Hussein Awadhi (5) MkaziwaKigogoBuyunina

3.BakariAwadhi (14), MkaziwaKigogoBuyuni

Watoto hao walifariki dunia kwa kusombwa na maji baada ya nyumba yao iliyopo katika bonde la Kigogo kujaa maji na watoto hao kushindwa kujiokoa na marehemu Ibrahim Hassani alijaribu kumuokoa mtoto mmoja lakini na yeye akasombwa na maji na kufariki dunia.

”Mnamotarehe 14 Oktoba, 2020 majira ya saa mbili asubuhi huko Mabibo mwili wamtu mmoja mwanaume asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati yamiaka 30-35  ulionekana unaelea kwenye mfereji unaopeleka maji katika mto Msimbazi, Miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali yaTaifa Muhimbili” Kamamda Mambosasa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *