Murray arejea kwa kishindo US OPEN, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 2, 2020 at 8:00 am

September 2, 2020

Muingereza Andy Murray alicheza mechi yake ya kwanza ya Grand Slam tangu mwaka 2019 na kushinda dhidi Mjapan Yoshihito Nishioka katika mchezo wake wa raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Marekani.Kwa mara ya mwisho Murray kushiriki michuano ya Grand Slam ilikua ni kwenye michuano ya wazi ya Australia mwaka jana mwezi Januari,alishinda kwa seti tano 4-6 4-6 7-6 (7-5) 7-6 (7-4) 6-4 akitumia masaa manne na dakika arobaini na nane.Murray alitumia siku596 kuuguza majeraha ya nyonga na sasa yeye na Dovak Djokovic ndio nyota wanaopewa nafasi ya kutwaa taji la US Open kutokana na kukosekana kwa Roger Federer aliye majeruhi na Bingwa mtetezi Rafael Nadal ambaye alijiondoa kwa hofu ya Corona.Kwa upande wa wanawake Johanna Conta amefuzu raundi ya pili kwa kumshinda Hearther Watson kwa seti 7-6 (9-7) 6-1.,

Muingereza Andy Murray alicheza mechi yake ya kwanza ya Grand Slam tangu mwaka 2019 na kushinda dhidi Mjapan Yoshihito Nishioka katika mchezo wake wa raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Marekani.

Kwa mara ya mwisho Murray kushiriki michuano ya Grand Slam ilikua ni kwenye michuano ya wazi ya Australia mwaka jana mwezi Januari,alishinda kwa seti tano 4-6 4-6 7-6 (7-5) 7-6 (7-4) 6-4 akitumia masaa manne na dakika arobaini na nane.

Murray alitumia siku596 kuuguza majeraha ya nyonga na sasa yeye na Dovak Djokovic ndio nyota wanaopewa nafasi ya kutwaa taji la US Open kutokana na kukosekana kwa Roger Federer aliye majeruhi na Bingwa mtetezi Rafael Nadal ambaye alijiondoa kwa hofu ya Corona.

Kwa upande wa wanawake Johanna Conta amefuzu raundi ya pili kwa kumshinda Hearther Watson kwa seti 7-6 (9-7) 6-1.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *