Muhamiaji mwanamke mwenye virusi vya corona ajifungua ndani ya helikopta, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 2, 2020 at 1:00 pm

September 2, 2020

 Muhamiaji mwanamke ambaye alipatikana na virusi vya corona baada ya kupimwa amejifungua mtoto ndani ya helikoptawa wakati alipokuwa alisafirishwa kwenda hospitali kutoka kwenye kituo cha wahamiaji nchini Italia kilichopo katika kisiwa cha Lampedusa.Italia inasema kuwa imeshuhudia ongezeko la wahamiaji wanaowasili mwaka huu.Meli ya uokozi ilipewa ruhusa Jumanne kuwasafirisha wahamiaji 353 waliookolewa kwenye kisiwa cha Sicily baada ya kupigiwa simu na Umoja wa Mataifa ulioitaka iwaokoe.Wakati huo huo, meli ya mafuta iliyokuwa na wahamiaji 27 ndani yake imeomba upya isaidiwe kuwafikisha wahamiaji kwenye mwambao wa Italia.Meli ya hiyo ya kibiashara , Maersk Etienne, inasema iliwaokoa wahamiaji hao kufuatia ombi la Malta mapema mwezi Agosti lakini tangu wakati huo imeachwa baharini. Wafanyakazi wake wanasema watu waliomo “wana hali mbaya”.Mwanamke alikuwa amepatikana na virusi vya corona wakati alipopata uchungu wa uzazi.Alikuwa anaishi katika kituo kinachowashikilia wahamiaji ambacho kilikuwa kimejaa wahamiaji mara kumi ya uwezo wake wa kawaida, kulingana taarifa za shirika la habari la Reuters.Maafisa wanasema waliamua kumuhamishia katika hospitali ya mji mkuu wa Sicily Palermo -ambayo ilikuwa umbali wa mwendo wa saa moja kwakwa ndege – ili aweze kujifungua kwa usalama. Lakini akajifungua safarini ndani ya ndege.Mwanamke huyo ambaye bado hajatambuliwa-kwa sasa yuko katika hospitali ya Palermo pamoja na mtoto wake mchanga.Tukio hilo limetokea huku kukiwa na mzozo baina ya watawala wa kisiwa cha Sicily na serikali ya taifa, huku Gavana wa Sicily Nello Musumeci akiishutumu serikali kuu ya Roma kwa kutompatia msaada wa kutosha wa kushughulikia wahamiaji wanaowasili kutoka Afrika.Wahamiaji wapatao 19,400 wamewasili kwenye maeneo ya mwambao wa Italia hadi sasa mwaka huu, ikilinganishwa na wahamiaji wapatao 5,200 waliowasili katika kipindi sawa na hicho mwaka jana, kwa mujibu wa taarifa zilizoangaliwa na shirika la habari la Reuters.Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya 40,000 wamewasili Ulaya kupitia baharini katika 2020 na watu 443 wamekufa au wamepotea walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean wakitokea Afrika magharibi.,

 

Muhamiaji mwanamke ambaye alipatikana na virusi vya corona baada ya kupimwa amejifungua mtoto ndani ya helikoptawa wakati alipokuwa alisafirishwa kwenda hospitali kutoka kwenye kituo cha wahamiaji nchini Italia kilichopo katika kisiwa cha Lampedusa.

Italia inasema kuwa imeshuhudia ongezeko la wahamiaji wanaowasili mwaka huu.

Meli ya uokozi ilipewa ruhusa Jumanne kuwasafirisha wahamiaji 353 waliookolewa kwenye kisiwa cha Sicily baada ya kupigiwa simu na Umoja wa Mataifa ulioitaka iwaokoe.

Wakati huo huo, meli ya mafuta iliyokuwa na wahamiaji 27 ndani yake imeomba upya isaidiwe kuwafikisha wahamiaji kwenye mwambao wa Italia.

Meli ya hiyo ya kibiashara , Maersk Etienne, inasema iliwaokoa wahamiaji hao kufuatia ombi la Malta mapema mwezi Agosti lakini tangu wakati huo imeachwa baharini. Wafanyakazi wake wanasema watu waliomo “wana hali mbaya”.

Mwanamke alikuwa amepatikana na virusi vya corona wakati alipopata uchungu wa uzazi.

Alikuwa anaishi katika kituo kinachowashikilia wahamiaji ambacho kilikuwa kimejaa wahamiaji mara kumi ya uwezo wake wa kawaida, kulingana taarifa za shirika la habari la Reuters.

Maafisa wanasema waliamua kumuhamishia katika hospitali ya mji mkuu wa Sicily Palermo -ambayo ilikuwa umbali wa mwendo wa saa moja kwakwa ndege – ili aweze kujifungua kwa usalama. Lakini akajifungua safarini ndani ya ndege.

Mwanamke huyo ambaye bado hajatambuliwa-kwa sasa yuko katika hospitali ya Palermo pamoja na mtoto wake mchanga.

Tukio hilo limetokea huku kukiwa na mzozo baina ya watawala wa kisiwa cha Sicily na serikali ya taifa, huku Gavana wa Sicily Nello Musumeci akiishutumu serikali kuu ya Roma kwa kutompatia msaada wa kutosha wa kushughulikia wahamiaji wanaowasili kutoka Afrika.

Wahamiaji wapatao 19,400 wamewasili kwenye maeneo ya mwambao wa Italia hadi sasa mwaka huu, ikilinganishwa na wahamiaji wapatao 5,200 waliowasili katika kipindi sawa na hicho mwaka jana, kwa mujibu wa taarifa zilizoangaliwa na shirika la habari la Reuters.

Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya 40,000 wamewasili Ulaya kupitia baharini katika 2020 na watu 443 wamekufa au wamepotea walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean wakitokea Afrika magharibi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *