Mtwara: Wanawake kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakinyimwa haki ya kumiliki mali,

October 6, 2020

 Mtwara;Wanawake kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakinyimwa haki ya kumiliki mali.

Na Faruku Ngonyani, Mtwara

Kutokana na hali ya kiuchumi kwa baadhi ya Wanawake Mkoani Mtwara  imepelekea wengi wao kupoteza haki zao za msingi pindi wanapokuwa wanatengana na waume zao.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirirka la Door of Hope Clemence Mwombeki,Taasisi inayofanya kazi ya Utetezi ,Uwezeshaji na Usaidizi wa Wananwake na Vijana hapa Nchini.

Mwombeki amesema kuwa kwa sasa kesi ambazo zimekuwa zikiripotiwa kwenye ofisi yake ni pamoja na Talaka holela haswa nyakati hizi za kuelekea msimu wa zao la korosho,ambapo wanaume walio wengi wanawaacha wanawake wao na kuoa wananwake wengine.

Aidha amesema kuwa mara baada kuachana wanawake hao wamekuwa wakipewa mali kidogo kutokana na hali yao kiuchimu huku wanaume hao hutumia pesa zao kuwakandamiza wanawake hao

Aidha Mwombeki amezungumzia juu ya Mila na desturi zinavyoathili watoto hususani Unyago ambapo mtoto wa darasa la sita au la saba anapokuwa anafundishwa namna ya kumuhudmia mwanaume inawapelekea kwenda kufanya majaribio na kupelekea kupata ujauzito na kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Aidha Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wazazi na walezi kutafuta njia mbadala ya unyago ili kuwanusuru watoto hoa kujiingiza kwenye mahusuiano ya kimapenzi mapema..

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *