Mtoto wa Miaka Mitano Alivyowakazia Wezi Wenye Silaha Nyumbani

October 19, 2020

 

Mtoto wa miaka mitano huko Indiana Marekani aligoma kuwakimbia Wezi pale walipovamia nyumbani kwao akiwa na Mama yake, alibaki kuwasumbua hadi walipoondoka, Wezi hao walivamia kwenye nyumba hiyo wakiwa wanne huku watatu kati yao wakiwa na silaha.

Wakati Mama yake alipokimbia kwenda kutafuta msaada, Mtoto huyo hakwenda popote bali alibaki eneo la tukio akijaribu kuwafukuza Wezi hao kwa kuwarushia vitu vyake vya kuchezea ambapo baada ya kuona hawatoki, aliamua kudandia mkono wa Mwizi mmoja kati yao 

Hata hivyo hivyo Wezi hao hawakutaka kumdhuru Mtoto huyo kwa chochote na walimchukulia kama Mtoto tu, Mama yake Mzazi amesema Mwanae alimwambia hakuwa anaogopa chochote na alikua anamlinda Mama dhidi ya lolote baya ambalo Wezi wangeweza kulifanya, tazama hii video hapa chini kutazama.

Mtoto wa miaka mitano alivyowakazia Wezi wenye silaha nyumbani (+video) ,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *