Mtatiro ataka ujenzi wa stendi ya Tunduru ufanywe kwa saa 24, on September 8, 2020 at 8:00 am

September 8, 2020

 Mkuu wa Wilaya wa Tunduru Julius Mtatiro amewaelekeza wahandisi na wakandarasi wanaokarabati stendi ya mabasi ya mjini Tunduru kukamilisha ukarabati huo kwa siku zisizozidi 30 badala ya kutumia siku 45 zilizoombwa na mhandisi wa halmashauri na wataalamu wengine.Mtatiro ameelekeza hayo alipotembelea eneo la stendi leo na kukuta hakuna kazi zinazofanyika licha ya halmashauri kuwaondoa wafanyabiashara tangu tarehe 05 Septemba.Mtatiro ameshangazwa na hali hiyo na kueleza kuwa anajua Mkurugenzi wake alikwishatenga fedha za kazi hiyo na kwamba kama ujenzi haujaanza kuna mtu atakuwa hajatimiza wajibu wake.”Fungeni taa na fanyeni kazi usiku na mchana, siku 45 mlizoomba zitapungua mara mbili kwa hiyo baada ya siku 22 ntakuja kukagua, nikute kazi zilizobakia ni za umaliziaji tu” alisema Mtatiro.Katika hatua nyingine Mtatiro amefuta ada ya shilingi 1,000 ambayo wafanyabiashara wanatozwa ili kugawiwa maeneo ya kufanyia biashara kwenye stendi ya muda.Kama hiyo haitoshi Mtatiro amefuta pia ada ya shilingi 30,000 ambayo wafanyabishara wametozwa kama ada ya kupewa eneo jipya la biashara la kutumia kwa muda mfupi.Mtatiro ameagiza wafanyabiashara wote waliotozwa fedha hizo warejeshewe ndani ya siku tatu.Wafanyabiashara wa Tunduru wamefurahia sana uamuzi huo na baadhi yao wamekiri kuwa serikali inapasea kuendelea kuwatetea katika mazingira kama hayo yanayowakabili.,

 

Mkuu wa Wilaya wa Tunduru Julius Mtatiro amewaelekeza wahandisi na wakandarasi wanaokarabati stendi ya mabasi ya mjini Tunduru kukamilisha ukarabati huo kwa siku zisizozidi 30 badala ya kutumia siku 45 zilizoombwa na mhandisi wa halmashauri na wataalamu wengine.

Mtatiro ameelekeza hayo alipotembelea eneo la stendi leo na kukuta hakuna kazi zinazofanyika licha ya halmashauri kuwaondoa wafanyabiashara tangu tarehe 05 Septemba.

Mtatiro ameshangazwa na hali hiyo na kueleza kuwa anajua Mkurugenzi wake alikwishatenga fedha za kazi hiyo na kwamba kama ujenzi haujaanza kuna mtu atakuwa hajatimiza wajibu wake.

“Fungeni taa na fanyeni kazi usiku na mchana, siku 45 mlizoomba zitapungua mara mbili kwa hiyo baada ya siku 22 ntakuja kukagua, nikute kazi zilizobakia ni za umaliziaji tu” alisema Mtatiro.

Katika hatua nyingine Mtatiro amefuta ada ya shilingi 1,000 ambayo wafanyabiashara wanatozwa ili kugawiwa maeneo ya kufanyia biashara kwenye stendi ya muda.

Kama hiyo haitoshi Mtatiro amefuta pia ada ya shilingi 30,000 ambayo wafanyabishara wametozwa kama ada ya kupewa eneo jipya la biashara la kutumia kwa muda mfupi.

Mtatiro ameagiza wafanyabiashara wote waliotozwa fedha hizo warejeshewe ndani ya siku tatu.

Wafanyabiashara wa Tunduru wamefurahia sana uamuzi huo na baadhi yao wamekiri kuwa serikali inapasea kuendelea kuwatetea katika mazingira kama hayo yanayowakabili.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *