Msumbiji yapinga madai ya Amnesty International kuwa inawatesa wafungwa, on September 11, 2020 at 10:00 am

September 11, 2020

 Jeshi la Msumbiji limekanusha tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu iliyotolewa dhidi yake na shirika la kutetea haki la Amnesty International kufuatia juhudi zake za kukabiliana na wanamgambo wa kiislamu katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa nchi hiyo.Mapema wiki hii Amnesty International iliwalaumu wanajeshi wa Msumbiji kwa kuekeleza mauaji, na kuwatesa wafungwa wanaoazuiliwa katika kile kinadai kuwa mauaji ya kiholela na kusafirisha idadi kubwa ya maiti na kuzizika katika makaburi ya pamoja.Shirika hilo linatumia ushahidi ambao linasema ni kanda ya video na picha ambazo “limethibitisha” kutoka eneo hilo zikionesha uhalifu unaotekelezwa dhidi ya wafungwa wanaozuiliwa na maafisa hao.Lakini msemaji wa wizara ya ulinzi ya Msumbiji, Omar Saranga, anasema Amnesty haikuzingatia picha hizo huenda zimetolewa na waasi ili kudhalilisha jeshi.Pia amelishutumu Amnesty International kwa “kukaa kimya dhidi ya unyama ambao umekuwa ukitekelezwa katika mkoa wa Cabo Delgado tangu 2017”.,

 

Jeshi la Msumbiji limekanusha tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu iliyotolewa dhidi yake na shirika la kutetea haki la Amnesty International kufuatia juhudi zake za kukabiliana na wanamgambo wa kiislamu katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa nchi hiyo.

Mapema wiki hii Amnesty International iliwalaumu wanajeshi wa Msumbiji kwa kuekeleza mauaji, na kuwatesa wafungwa wanaoazuiliwa katika kile kinadai kuwa mauaji ya kiholela na kusafirisha idadi kubwa ya maiti na kuzizika katika makaburi ya pamoja.

Shirika hilo linatumia ushahidi ambao linasema ni kanda ya video na picha ambazo “limethibitisha” kutoka eneo hilo zikionesha uhalifu unaotekelezwa dhidi ya wafungwa wanaozuiliwa na maafisa hao.

Lakini msemaji wa wizara ya ulinzi ya Msumbiji, Omar Saranga, anasema Amnesty haikuzingatia picha hizo huenda zimetolewa na waasi ili kudhalilisha jeshi.

Pia amelishutumu Amnesty International kwa “kukaa kimya dhidi ya unyama ambao umekuwa ukitekelezwa katika mkoa wa Cabo Delgado tangu 2017”.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *