Msonde aeleza sababu za kuchaguliwa Magufuli, on September 13, 2020 at 1:00 pm

September 13, 2020

Na Omary Mngindo, Yombo.MENEJA Kampeni wa Ubunge Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Yahya Msonde, amewataka wa-Tanzania kumchagua kwa kura nyingi Dkt. John Magufuli, ili kulipa fadhira kutokana na kazi kubwa anayoifanya.Msonde alisema kuwa Dkt. Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano, amesimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato katika mashirika na Taasisi mbalimbali, kutoka sifuri mpaka sasa yanalipa shilingi Tririon 1.052 kwa mwaka.Aidha kupitia Madini, Rais huyo ambae ndio Mwenyekiti wa chama hicho ambae ameomba tena ridha kwa wa-Tanzania, amewezesha kupatikana kwa shilingi bii. 346 kutoka bil. 168 kutoka sekra hiyo zilizokuwa zikikusanywa kabla ya mwaka 2015.”Ndugu zangu wana-Yombo na wa-Tanzania tunapaswa kuilinda tunu hii tuliyobalikiwa na Mwenyezimungu, Dkt. Magufuli kabla hatujaingia madarakani mashirika yalikuwa hayalipi kodi, sanjali madini, alipoingia 2015 kipindi cha 2015 mashirika yanalipa Tririon 1.052, huku upande wa Madini yakiongezeka kutoka Bil. 168 mpaka 346 kwa mwaka,” alisema Msonde.Kwa upandea wake Mkenge alimpongeza mtangulizi wake Dkt. Shukuru Kawambwa, akisema kuwa akishirikiana na viongozi wenzake wameyafanya mengi makubwa, huku akiwaomba wana-Bagamoyo kuwachagua wagombea sanaotokea CCM.”Mkimchagua Dkt. John Magufuli, Mimi ndugu yenu Mkenge na Mohamed Usinga udiwani, mtakuwa mmeweka safu nzuri itayoendeleza mazuri ambayo tayari Serikali inayomaliza muda wake imeshaanza kuyafanya,” alisema Mkenge.Akizungumzia ajira, Mkenge alisema kwamba kuna baadhi ya vijiji vina fursa nzuri ya kilimo cha umwagiliaji, kutokana na kuwepo mito inayopitisha maji, hivyo watahakikisha wanawezesha mashine za kumwagilia, kukuza kilimo hicho huku akisema kuwa kuna soko kubwa la bidhaa za mbogamboga. “Wana-Yombo na Bagamoyo nimwombee kura mgombea wetu wa urais Dkt. John Magufuli, mimi Mkenge na Udiwani Usinga ili kwa umoja wetu tuboreshe tuliyoyaanzisha, hapa Yombo kuna Kituo cha afya kinahitaji kuendelezwa na miradi mbalimbali,” alimalizia Mkenge.Nae Usinga alisema kwamba ndani ya Yombo kuna miradi kadhaa imeshatekelezwa ikiwemo ya maji, umeme, zahanati sanjali uboreshaji was shule za msingi, huku akisema sekondari ya Miembesaba imepanda hadhi na kuwa ya kidato tano na sita. ,

Na Omary Mngindo, Yombo.

MENEJA Kampeni wa Ubunge Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Yahya Msonde, amewataka wa-Tanzania kumchagua kwa kura nyingi Dkt. John Magufuli, ili kulipa fadhira kutokana na kazi kubwa anayoifanya.

Msonde alisema kuwa Dkt. Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano, amesimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato katika mashirika na Taasisi mbalimbali, kutoka sifuri mpaka sasa yanalipa shilingi Tririon 1.052 kwa mwaka.

Aidha kupitia Madini, Rais huyo ambae ndio Mwenyekiti wa chama hicho ambae ameomba tena ridha kwa wa-Tanzania, amewezesha kupatikana kwa shilingi bii. 346 kutoka bil. 168 kutoka sekra hiyo zilizokuwa zikikusanywa kabla ya mwaka 2015.

“Ndugu zangu wana-Yombo na wa-Tanzania tunapaswa kuilinda tunu hii tuliyobalikiwa na Mwenyezimungu, Dkt. Magufuli kabla hatujaingia madarakani mashirika yalikuwa hayalipi kodi, sanjali madini, alipoingia 2015 kipindi cha 2015 mashirika yanalipa Tririon 1.052, huku upande wa Madini yakiongezeka kutoka Bil. 168 mpaka 346 kwa mwaka,” alisema Msonde.

Kwa upandea wake Mkenge alimpongeza mtangulizi wake Dkt. Shukuru Kawambwa, akisema kuwa akishirikiana na viongozi wenzake wameyafanya mengi makubwa, huku akiwaomba wana-Bagamoyo kuwachagua wagombea sanaotokea CCM.

“Mkimchagua Dkt. John Magufuli, Mimi ndugu yenu Mkenge na Mohamed Usinga udiwani, mtakuwa mmeweka safu nzuri itayoendeleza mazuri ambayo tayari Serikali inayomaliza muda wake imeshaanza kuyafanya,” alisema Mkenge.

Akizungumzia ajira, Mkenge alisema kwamba kuna baadhi ya vijiji vina fursa nzuri ya kilimo cha umwagiliaji, kutokana na kuwepo mito inayopitisha maji, hivyo watahakikisha wanawezesha mashine za kumwagilia, kukuza kilimo hicho huku akisema kuwa kuna soko kubwa la bidhaa za mbogamboga.

 “Wana-Yombo na Bagamoyo nimwombee kura mgombea wetu wa urais Dkt. John Magufuli, mimi Mkenge na Udiwani Usinga ili kwa umoja wetu tuboreshe tuliyoyaanzisha, hapa Yombo kuna Kituo cha afya kinahitaji kuendelezwa na miradi mbalimbali,” alimalizia Mkenge.

Nae Usinga alisema kwamba ndani ya Yombo kuna miradi kadhaa imeshatekelezwa ikiwemo ya maji, umeme, zahanati sanjali uboreshaji was shule za msingi, huku akisema sekondari ya Miembesaba imepanda hadhi na kuwa ya kidato tano na sita.

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *