Mshauri wa Ikulu ya Whitehouse aambukizwa corona, huku viongozi wa kijeshi wakijiweka karantini,

October 7, 2020

Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kusambaa miongoni mwa wandani wa Rais wa Marekani Donald Trump, huku mshauri wa Ikulu ya White House Stephen Miller na afisa wa jeshi wa ngazi ya juu wakithibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Bw. Miller, ambaye alikuwa amejitenga kwa situ tano, amethibitisha kuwa na virusi hivyo Jumanne.

Jenerali wa ngazi ya juu wa jeshi la Marekani Mark Milley na viongozi wangine wa kijeshi pia wamewekwa karantini baada afisa wa ulinzi wa pwani Admiral Charles Ray kupatikana na corona.

Maaafisa wengine wamejitenga “kama hatua ya kujilinda”.

Katika taarifa, Bw. Miller alisema matokeo ya uchunguzi wake “yamekuwa yakionesha hana kila siku” hadi Jumanne, akiongeza kuwa sasa yuko karantini.

Mke wake, Katie Miller, ambaye ni msemaji wa Makamu wa Rais Mike Pence, aliambukizwa virusi hivyo mwezi Mei lakini akapona baadae.

Mwezi Julai, Bibi yake Bw Miller mwenye ummri wa miaka 97, Ruth Glosser, aliripotiwa kufariki dunia kutokana na changamoto za kiafya zilizosababishwa na ugonjwa wa Covid-19.

Ikulu ya White House ilikanusha madai kwamba virusi vya corona vilisababisha kifo cha Bi Glosser, ikisema Katika taarifa kwamba “alipumzika kwa amani kutokana na uzee”.

Ikulu ya White House ilikanusha madai kwamba virusi vya corona vilisababisha kifo cha Bi Glosser, ikisema Katika taarifa kwamba “alipumzika kwa amani kutokana na uzee”.

Lakini mjomba wa Bw. Miller alitoa cheti cha kifo kilichoonesha “tatizo la kupumua” na Covid-19 kama “hali iliyochangia” kifo cha Bi Glosser.

Bw. Miller – ambaye huandika hotuba za rais – anajulikana kwa misimamo yake mikali kuhusu masuala ya uhamiaji.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *