Mserbia Yanga SC Ampa Shavu Carlinhos

September 10, 2020

KOCHA wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema ataanza kumtumia kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos katika michezo inayofuata ya ligi kuu.Carlinhos ambaye amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea nchini Angola, ameshindwa kupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa sare ya 1-1.Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo alisema Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila bado hajawa tayari kucheza kutokana na kukosa utimamu wa mechi, lakini karibuni anatarajiwa kuwa fiti.“Carlinhos ni mchezaji mzuri, tunatarajia kupata ufundi wake hivi karibuni lakini kwa sasa hajaonekana uwanjani kwa kuwa bado hana utimamu wa mwili katika kucheza mechi ila hivi karibuni ataonekana uwanjani.“Ukiachana na yeye pia bado kuna wachezaji wengi ambao hawajawa fiti lakini tunatarajia kupata ubora wao huko mbeleni kwa kuwa wanahitaji muda kuonyesha ubora wao,” alisema kocha huyo.Yanga inatarajia kumenyana na Mbeya City katika mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu utakaofanyika Jumapili, Septemba 13, katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam,

KOCHA wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema ataanza kumtumia kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos katika michezo inayofuata ya ligi kuu.

Carlinhos ambaye amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea nchini Angola, ameshindwa kupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo alisema Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila bado hajawa tayari kucheza kutokana na kukosa utimamu wa mechi, lakini karibuni anatarajiwa kuwa fiti.

“Carlinhos ni mchezaji mzuri, tunatarajia kupata ufundi wake hivi karibuni lakini kwa sasa hajaonekana uwanjani kwa kuwa bado hana utimamu wa mwili katika kucheza mechi ila hivi karibuni ataonekana uwanjani.

“Ukiachana na yeye pia bado kuna wachezaji wengi ambao hawajawa fiti lakini tunatarajia kupata ubora wao huko mbeleni kwa kuwa wanahitaji muda kuonyesha ubora wao,” alisema kocha huyo.

Yanga inatarajia kumenyana na Mbeya City katika mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu utakaofanyika Jumapili, Septemba 13, katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *