Msafara wa Tundu Lissu Wazuiwa Pwani

October 6, 2020

Jeshi la Polisi wenye silaha za moto na Mabomu ya machozi muda huu wameuzuia msafara wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tundu Lissu maeneo ya Kiluvya ukiwa unaelekea Kibaha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema, wamezuia msafara wa Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chadema kuendelea na ziara mkoani humo; “tunahofia usalama wake kwani amezuiliwa kufanya kampeni kwa siku saba. Amesema atakaa pale na sisi tutakesha naye.”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *