Mripuko mwingine wa moto wazusha taharuki Beirut, on September 10, 2020 at 5:00 pm

September 10, 2020

Taharuki imetanda katika mji mkuu wa Lebanon Beirut mapema leo, baada ya moto mkubwa kuzuka katika ghala kwenye bandari ya mji huo, mwezi mmoja tu baada ya kutokea mripuko mkubwa mahali hapo hapo. Jeshi la Lebanon limearifu kuwa moto huo ulitokea katika bohari la mafuta na matairi ya magari, na kuongeza kuwa limetuma helikopta kwenda kusaidia shughuli za kuuzima moto huo.Mtu aliyeshuhudia ameliambia shirika la habari la dpa kuwa wafanyakazi katika majengo yaliyo karibu na bandari walipewa amri ya kuondoka haraka. Katibu Mkuu wa Shrika la Msalaba Mwekundu nchini Lebanon, George Kettnah amesema kuwa mtu mmoja alipata matatizo ya kupumua kutokana na moto huo, lakini hakuna madhara makubwa yaliyoripotiwa.Mripuko mkubwa wa Agosti nne kwenye bandari hiyo hiyo uliwauwa watu 190 na kuwajeruhi wengine 6,000, na kuwaacha wapatao 300,000 bila makaazi.,

Taharuki imetanda katika mji mkuu wa Lebanon Beirut mapema leo, baada ya moto mkubwa kuzuka katika ghala kwenye bandari ya mji huo, mwezi mmoja tu baada ya kutokea mripuko mkubwa mahali hapo hapo. Jeshi la Lebanon limearifu kuwa moto huo ulitokea katika bohari la mafuta na matairi ya magari, na kuongeza kuwa limetuma helikopta kwenda kusaidia shughuli za kuuzima moto huo.

Mtu aliyeshuhudia ameliambia shirika la habari la dpa kuwa wafanyakazi katika majengo yaliyo karibu na bandari walipewa amri ya kuondoka haraka. Katibu Mkuu wa Shrika la Msalaba Mwekundu nchini Lebanon, George Kettnah amesema kuwa mtu mmoja alipata matatizo ya kupumua kutokana na moto huo, lakini hakuna madhara makubwa yaliyoripotiwa.

Mripuko mkubwa wa Agosti nne kwenye bandari hiyo hiyo uliwauwa watu 190 na kuwajeruhi wengine 6,000, na kuwaacha wapatao 300,000 bila makaazi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *