Moto wa porini wateketeza kilomita mraba 8000 California, on September 8, 2020 at 6:00 pm

September 8, 2020

Moto mkubwa wa mwituni umeangamiza zaidi ya kilomita 8000 za mraba katika jimbo la California nchini Marekani.Wizara ya misitu na ulinzi dhidi ya moto nchini humo imesema huu ndio moto mbaya zaidi kuwahi kurekodiwa tangu mwaka 1987.Kusini mwa jimbo la California, wakazi walishauriwa kuziacha nyumba zao zinazonyemelewa na moto huo na kutafuta hifadhi mahali salama. Upande wa kaskazini wa jimbo hilo, watu wapatao 200 waliokolewa na helikopta za kijeshi, baada moto huo kuuzingira kwa kasi mji wa Fresno.,

Moto mkubwa wa mwituni umeangamiza zaidi ya kilomita 8000 za mraba katika jimbo la California nchini Marekani.

Wizara ya misitu na ulinzi dhidi ya moto nchini humo imesema huu ndio moto mbaya zaidi kuwahi kurekodiwa tangu mwaka 1987.

Kusini mwa jimbo la California, wakazi walishauriwa kuziacha nyumba zao zinazonyemelewa na moto huo na kutafuta hifadhi mahali salama. Upande wa kaskazini wa jimbo hilo, watu wapatao 200 waliokolewa na helikopta za kijeshi, baada moto huo kuuzingira kwa kasi mji wa Fresno.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *