Moto wa misitu wasababisha vifo Ukraine,

October 3, 2020

 

Watu 11 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 7 kujeruhiwa kwenye moto mkali uliotokea sehemu 146 za msitu katika eneo la Lugansk lililoko mashariki mwa Ukraine.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine,  iliarifiwa kuwa moto huo wa misitu uliweza kuzimwa katika sehemu 116 huku juhudi ya kuzima sehemu nyingine 30 ikiendelea.

Watu 120 wameweza kuhamishwa kutokana na moto huo.

Majengo 250 yanaarifiwa kuharibiwa kutokana na moto huo ulioenea na kuteketeza hekari elfu 11.

Idara ya Polisi ya Ukraine imeanzisha  uchunguzi  kuhusu chanzo cha moto huo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *