Mo Dewji ashindwa kuvumilia, aamua kuwachukulia hatua wanaotumia jina lake kumchafua, on September 17, 2020 at 1:00 pm

September 17, 2020

  Kutokana na hali inayoendelea katika mitandao ya kijamii, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, amecharuka na kusema amepanga kuchukua hatua za kisheria kwa watu wanaotumia jina lake kumchafua.Hivi karibuni baada ya Mo Dewji kuhusishwa kutumia kaunti yake ya twitter kumjibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala ambaye pia ni shabiki wa Simba akihoji kuhusu shilingi bilioni 20 za uwekezaji, kumekuwa na muendelezo wa maneno mbalimbali yanayoandikwa katika akaunti anayodai ni feki ikitumia jina lake.Hali hiyo imekuwa ikizua taharuki kwa wapenzi na wadau wa klabu hiyo na kuleta mkanganyiko ndani ya Simba, huku wengi wakichukulia maneno hayo ni kweli yanatoka kwa bosi wao huyo.Kutokana na hali hiyo kukithiri,  Mo Dewji ameamua kutoa ya moyoni na kusema uvumilivu umemshinda na lazima atachukua hatua za kisheria dhidi ya wale wanaotengeneza akaunti feki za kumchafua, yeye na jina la klabu ya Simba.Katika akaunti zake za mitandaoni, Mo aliandika kuwa hahusiki na akaunti hizo zinazoleta taharuki kwa Wanasimba na anafuatilia kwa umakini kujua mhusika wa hilo.,

 

Kutokana na hali inayoendelea katika mitandao ya kijamii, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, amecharuka na kusema amepanga kuchukua hatua za kisheria kwa watu wanaotumia jina lake kumchafua.

Hivi karibuni baada ya Mo Dewji kuhusishwa kutumia kaunti yake ya twitter kumjibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala ambaye pia ni shabiki wa Simba akihoji kuhusu shilingi bilioni 20 za uwekezaji, kumekuwa na muendelezo wa maneno mbalimbali yanayoandikwa katika akaunti anayodai ni feki ikitumia jina lake.

Hali hiyo imekuwa ikizua taharuki kwa wapenzi na wadau wa klabu hiyo na kuleta mkanganyiko ndani ya Simba, huku wengi wakichukulia maneno hayo ni kweli yanatoka kwa bosi wao huyo.

Kutokana na hali hiyo kukithiri,  Mo Dewji ameamua kutoa ya moyoni na kusema uvumilivu umemshinda na lazima atachukua hatua za kisheria dhidi ya wale wanaotengeneza akaunti feki za kumchafua, yeye na jina la klabu ya Simba.

Katika akaunti zake za mitandaoni, Mo aliandika kuwa hahusiki na akaunti hizo zinazoleta taharuki kwa Wanasimba na anafuatilia kwa umakini kujua mhusika wa hilo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *