MO Ampa Kazi Maalum Morrison Simba

September 9, 2020

MWENYEKITI wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya soka ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ amesema kuwa tayari uongozi wa klabu hiyo wamekaa chini na wachezaji wao wote pamoja na benchi la ufundi chini ya Mbelgiji, Sven Vandenbroeck na kuwaeleza kuwa malengo yao makubwa msimu huu ni kuhakikisha wanatwaa taji la nne mfululizo la Ligi Kuu BaraMwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya soka ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’.Simba imefanya usajili wa wachezaji wapya saba ambao sasa wanaunda kikosi cha wachezaji 29, watakaokuwa na kibarua kizito mbele ya wapinzani wao katika harakati za kutetea taji la Ligi Kuu Bara msimu huu na walianza vizuri kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu.Akizungumzia malengo yao makubwa msimu huu kupitia mtandao wa You tube wa timu hiyo, MO amesema: “Malengo ya klabu yetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi kwenye michuano ya kimataifa na ili kuweza kufanya hivyo basi hatuna budi kuhakikisha kuwa tunatetea tena ubingwa wa Ligi Kuu Bara.“Tayari tumekaa na wachezaji wetu pamoja na kocha mkuu, Sven Vandenbroeck na kuongea nao juu ya hili nao wameahidi kupambana licha ya ushindani uliopo ili kuifanya Simba ifi kie malengo ya kutwaa ubingwa kwa mara ya nne,” alisema MO.Baadhi ya wachezaji ambao wanadaiwa kukutana na Mo ni pamoja na Bernand Morrison, John Bocco, Aishi Manula, Mohamed Hussein Tshabalala, Larry Bwalya na wengine wengi.,

MWENYEKITI wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya soka ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ amesema kuwa tayari uongozi wa klabu hiyo wamekaa chini na wachezaji wao wote pamoja na benchi la ufundi chini ya Mbelgiji, Sven Vandenbroeck na kuwaeleza kuwa malengo yao makubwa msimu huu ni kuhakikisha wanatwaa taji la nne mfululizo la Ligi Kuu Bara

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya soka ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’.

Simba imefanya usajili wa wachezaji wapya saba ambao sasa wanaunda kikosi cha wachezaji 29, watakaokuwa na kibarua kizito mbele ya wapinzani wao katika harakati za kutetea taji la Ligi Kuu Bara msimu huu na walianza vizuri kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu.

Akizungumzia malengo yao makubwa msimu huu kupitia mtandao wa You tube wa timu hiyo, MO amesema: “Malengo ya klabu yetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi kwenye michuano ya kimataifa na ili kuweza kufanya hivyo basi hatuna budi kuhakikisha kuwa tunatetea tena ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

“Tayari tumekaa na wachezaji wetu pamoja na kocha mkuu, Sven Vandenbroeck na kuongea nao juu ya hili nao wameahidi kupambana licha ya ushindani uliopo ili kuifanya Simba ifi kie malengo ya kutwaa ubingwa kwa mara ya nne,” alisema MO.

Baadhi ya wachezaji ambao wanadaiwa kukutana na Mo ni pamoja na Bernand Morrison, John Bocco, Aishi Manula, Mohamed Hussein Tshabalala, Larry Bwalya na wengine wengi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *