Mnigeria, Mkorea kuchuana kuongoza WTO

October 8, 2020

Shirika la biashara duniani WTO, limesema waziri wa biashara wa Korea Kusini na msomi wa chuo kikuu cha Havard, waziri wa zamani wa fedha wa Nigeria wamefuzu kama wagombea wawili wa mwisho wa nafasi ya mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, na hivyo kuhakikisha mwanamke kushika nafsi hiyo ya juu kwa mara ya kwanza. 

Msemaji wa WTO Keith Rockwell, amesema leo kuwa kamati ya uteuzi iliwakuta Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria na Yoo Myung-hee wa Korea Kusini, kuwa wenye vigezo bora zaidi kwa ajili ya duru ya mwisho, kwenye mchuano unaotrajiwa kukamilika katika wiki zijazo. 

“Ripoti iliyotolewa na mwenyekiti wa Baraza kuu David Walker na wawezeshaji wenza wake, Balozi Aspelund na Balozi Castillo iliwasilishwa kwa wanachama leo, mapendekezo ni kwamba Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria, na waziri wa Korea Yoo Myung-hee watasonga mbele hadi hatua ya tatu na ya mwisho ya mashauriano,” alisema Rockwell. 

Baraza la WTO lenye makao yake mjini Geneva, Uswisi, linaloundwa na wajumbe kutoka chombo hicho chenye wanachama 164, liliwaondoa Amina Mohmed, waziri wa zamani wa biashara kutoka Kenya, Mohammed Maziad Al-Tuwaijiri, waziri wa zamani wa uchumi wa Saudi Arabia na waziri wa zamani wa biashara ya kimataifa wa Uingereza na mtetezi wa Brexit Liam Fox.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *