MNEC Anna awaomba kura wagombea wa CCM Kikwajuni,

October 10, 2020

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Ndugu Anna Msuya amewataka wananchi wa Zanzibar kuwachagua viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika oktoba 28 mwaka huu

Ametoa wito huo alipokua akihutubia mkutano wa jimbo la Kikwajuni uliofanyika katika uwanja wa kisonge Mjini Unguja wakati  akiwanadi wagombea wa jimbo hilo na kuwaombea kura

Anna amesema ni vyema wananchi wa jimbo la kikwajuni kuhakikisha wanawarudihsa tena madarakani viongozi wa jimbo hilo kutokana na maendeleo makubwa waliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wao sambamba na kuwahimiza katika kufanikisha ushindi wa ccm kwa kiti cha urais na majimbo yote nchini

Amesema kazi kubwa inayofanywa na serikali inayoongozwa na CCM ni moja ya alama ya kuwa chama hicho kinatoa viongozi walio bora na wenye Uzalendo wa kuleta Maendeleo Nchini

Akiomba kura kwa wananchi wa Kikwajuni Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Mhandisi Hamad Masauni amewahakikishia wananchi kuwa licha ya maendeleo makubwa aliyoyafanya katika awamu iliyopita ikwemo kutatua changamoto ya upatikanji wa maji safi na salama  pia amewaahidi kuwa kwa kipindi kijacho endapo atapata ridhaa tena ya kuongoza jimbo hilo atahakikisha anakabiliana na changamoto ya ajira kwa wananchi wa kikwajuni

“katika kipindi cha uongozi wangu niliahidi kukabiliana na tatizo la Maji na tayari nimefanikiwa kwa kuchukua juhudi mbalimbali ikiwemo kuanzisha miradi ya upatikanaji wa Maji Jimboni yenye gharama ya zaidi ya bilioni moja kwa mashirikiano ya wafadhili mbalimbali ndani na nje ya nchi na kwasa endapo mutatupa ridhaa ya kuongoza tena nitahakikisha tunakabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira ili kupunguza idadi ya wimbi kubwa la vijana ambao hawana ajira” alisema Masauni

Wagombea wengine wa jimbo la kikwajuni ni Nassor Salum Jazeera anaegombea nafasi ya uwakilishi,ibrahim khamis nafasi ya udiwani wadi ya kikwajuni na Mbarouk Abdulla Hanga nafasi ya udiwani wadi ya Rahaleo

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *