Mlemavu wa Miguu Mkoni Mtwara aomba kuonana na Mkuu wa Mkoa,

October 2, 2020

Na Faruku Ngonyani , Mtwara

Mlemavu wa Miguu anaefahamika kwa jina la Abeid Yususfu Lukanga Mkazi wa Mtaa wa Kiyangu kata ya Shangani Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara ameomba kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara au Mkuu wa Wilaya ili aweze kueleza chanagamoto ulizokuwananzo.

Abeid amabye pia Mjasirimali mdogo anaejishulisha na utengezeazji wa Baiskeli pamoja na ushonaji wa viatu  angependa kujiongeza kibiashara ili aweze kufikia malengo yake.

Awali  Abeid amesema kuwa alishwawahi kutengeneza bango kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tananzia Dkt John Pombe Magufuli  alipokuja Mkoani Mtwara Mwaka 2017, bango hilo lilisomeka “MHE RAIS JPM MIMI NI MLEMAVU NAFIKILI UMENIONA NIMEANZA MWENYEWE NAOMBA MSAADA WAKO KWAKO KWANI OMBA OMBA NI FEDHEAHA KWA JAMAII NA TAIFA KWA UJUMLA”

Amseema kuwa lengo la kuandika bango hilo ilikuwa ni kumuonesha Mh.Rais ili aweze kusaidiwa lakini hakupata nafasi ya kulionesha.

Kwa sasa Lukanga amesema kuwa kipato anachopata hakikidhi mahitaji yake hali inayopelekea baadhi ya vitu vyake kusimama kwa kukose pesa ya kuviendeleza.

Lengo la kuonana na Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa wilaya ili aweze kueleza chanagamoto alizonazo huku akiamini viongozi hao watamsikiliza na kuzitatua changamoto hizo

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *