Mlemavu aliyekaa ndani kwa miaka 8 apewa msaada wa baiskeli na wadau Mkoani Mtwara, on September 15, 2020 at 10:00 am

September 15, 2020

 Na Faruku Ngonyani, Mtwara.Mlemavu wa Miguu anayefahamika kwa jina la Nuru Ally Mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa Kata ya Mitengo Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara  amepatiwa  msaada wa baiskeli ya kutembelea.Nuru amevishukuru vyombo vya habari kwa kupaza sauti kwa wadau mbali mbali adi kufanikiwa kupatikana kwa baiskeli hiyo. Baiskeli hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Mtwara Mjini Ndg Yusufu Mpilu na kwa nafasi hiyo ametoa wito kwa wananchi wa Mtwara kwa yeyoye aliyeguswa na tukio hilo na ni vyema akatoa msaada kwa Nuru Ally kwani kwa sasa anahitaji msaada mbali mbali kama vile Nguo, chakula na mahitaji mengine ya kiubinadamu.Alisema alikuwa dereva pikipiki (boda boda) ambapo alipata ulemavu huo wa Miguu mwaka 2012 kwa  kupata ajali ya kugongwa na gari akiwa barabarani anaendsha pikipiki.Kwa upande wa mama mzazi wa Nuru Ally  Bi. Habiba saidi Selemani ameshukuru kwa msaada huo kwani awali ilikuwa changamoto kwa mtoto wake kutoka kwenda mbali na nyumbani kwake,kupatikana kwa baiskeli hiyo kutamrahisishia kuweza kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki.Nuru Ally ni Mkazi wa Mtaa wa kilimahewa uliopo kata ya Mitengo Manispaa Mtwara Mikindani na alipata ulemavu wa Miguu mwaka 2012 kwa kupata ajali ya kugongwa na gari akiwa barabarani anaendesha pikipiki. ,

 

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Mlemavu wa Miguu anayefahamika kwa jina la Nuru Ally Mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa Kata ya Mitengo Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara  amepatiwa  msaada wa baiskeli ya kutembelea.

Nuru amevishukuru vyombo vya habari kwa kupaza sauti kwa wadau mbali mbali adi kufanikiwa kupatikana kwa baiskeli hiyo. 

Baiskeli hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Mtwara Mjini Ndg Yusufu Mpilu na kwa nafasi hiyo ametoa wito kwa wananchi wa Mtwara kwa yeyoye aliyeguswa na tukio hilo na ni vyema akatoa msaada kwa Nuru Ally kwani kwa sasa anahitaji msaada mbali mbali kama vile Nguo, chakula na mahitaji mengine ya kiubinadamu.

Alisema alikuwa dereva pikipiki (boda boda) ambapo alipata ulemavu huo wa Miguu mwaka 2012 kwa  kupata ajali ya kugongwa na gari akiwa barabarani anaendsha pikipiki.

Kwa upande wa mama mzazi wa Nuru Ally  Bi. Habiba saidi Selemani ameshukuru kwa msaada huo kwani awali ilikuwa changamoto kwa mtoto wake kutoka kwenda mbali na nyumbani kwake,kupatikana kwa baiskeli hiyo kutamrahisishia kuweza kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki.

Nuru Ally ni Mkazi wa Mtaa wa kilimahewa uliopo kata ya Mitengo Manispaa Mtwara Mikindani na alipata ulemavu wa Miguu mwaka 2012 kwa kupata ajali ya kugongwa na gari akiwa barabarani anaendesha pikipiki. 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *