Mkurugenzi Mterndaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara aisistiza Makundi ya Akina Mama ,Vijana ,watu wenye ulemavu Kuchangamkia fursa ya Mikopo,

October 5, 2020

 

Na Faruku Ngonyani, Mtwara

Wananchi wa Kijiji cha Mkunwa kilichopopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara wameshauriwa  kuchangamkia fursa za kiuchumi ikiwepo uundwaji wa vikundi vya Vijana, akina Mama na Walemavu ili waweze kupata Mikopo ya 10% inayotolea na Halmashauri hiyo.

Wito huo umtolewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashasuri hiyo Bi Erica Yegella kwenye Mkutano wa Hadhara ulifanyika katika kijiji hiko cha Mkunwa.

Bi Yegella amesema kuwa kwa sasa ili wananchi waweze kujiongezeab kiuchumi na nimvyema wakachangamkia fursa ya kukopoa fedha hizo za Halmashauri , ambapo mpaka sasa bado kumekuwa na mwitikio mdogo haswa kwenye kundi la vijana.

Katika Mkutano hupo Wananchi wa kata ya  Mkunwa wakifuatilia kwa makini Rai ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Mtwara Erica E. Yegella wakati wa mkutano wa hadhara uliolenga kuimarisha Uhusiano Kati ya Watumishi na wananchi Siku ya Tarehe 02 Oktoba, 2020.

Mkurugenzin huyo ameendelea kuwakumbusha na kuwasisitia wananchi hao kuendelea kufanya usafi wa mazingira yao ili kata hiyo iweze kuendana na hadhi ya Makao Makuu ya Halmashri hiyo.

Ikumbwe kwa sasa Halmashauri zote hapa nchini zinapaswa kutenga aslimia Kumi (10%) ya mapato yao ya ndani ili kutoa mikopo kwa Makundi ya Akina Mama (4% ),Vijana (4%) na Watu wenye ulimavu (2%).

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *