Mkoa Wa Dodoma Watoa Vitambulisho Kwa Wazee Kwa Asilimia 76.chf Waongoza,

October 3, 2020

 

Zaidi ya  Wazee Milion moja kati ya Milioni mbili na laki tano nchi nzima tayari wamekwisha patiwa vitambulisho vitakavyowawezesha kupata huduma za Afya Bure huku Mkoa wa Dodoma Ukiongoza kwa kutoa vitambulisho kwa asilimia 76

Hayo yameelezwa Wilayani kondoa Mkoani Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt.John Jingu katiak maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani ambapo amesema kuwa lengo la Serikali ni kutoa huduma za Afya Bure kama Sera ya Wizara ya Afya inavyosema

“Hadi sasa kuna jitihada mbalimbali kuakikisha kuwa hilo linatekelezeka,kuna vile vitambulisho lakini pia kuna madirisha maalumu kwa ajili ya wazee yote hiyo ni kuhakikisha wazee wanathaminiwa na kupewa kipaymbele katika maeneo yote nchini”Alisema.

“Tunaendelea na jitihada hizo kuhakikisha kwamba wazee wetu katika maeneo yote nchini tunawatambua na kuwapatia vitambulisho ambavyo vitawawezesha kupata huduma za Afya bure na ninashukuru kwa kuwa Mkoa wa Dodoma unaongoza kwa hilo,inaonyesha kwamba mkiwa makao makuu mna wajibu na wajibu ni kuongoza,hongerni sana”Aliongeza

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Kessy Maduka yeye amesema kutokea katika Sera hiyo ya Wizara ya Afya yapo mambo mengi yaliyotekelezwa ikiwemo uboreshaji wa huduma lakini pia upatikanaji wake na kuhakikisha kuwa wazee wanapata huduma hizo bila malipo na kuwa Mkoa wa Dodoma umekuwa ukiongoza kwa kuhudumia wazee

“Mojawapo ni kwamba Dodoma ndio kinara wa uandikishaji wa familia katika mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ya CHF,sisi ndio tunaongoza tukiwa na asilimia karibu ishirini na Tano,kwahiyo Mkuu wa Mkoa ni kiongozi mzuri wa suala hili la kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya kwa makundi yote”Alisema

Naye Mratibu wa CHF Mkoa wa Dodoma Dkt.Francis Lutalala amesema kwa Mkoa wa Dodoma Serikali ya Awamu ya Tano imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya ili wananchi wakiwemo wazee waweze kupata huduma za Afya kwa gharama nafuu na pasipo kutembea kwa muda mrefu

Lutalala ameongeza kuwa pamoja na kuwa wazee wanatibiwa bure lakini wengine wanaishi na wategemezi ambao pindi wanapougua hulazimika kuwatafutia fedha za matibabu,hivyo basi Serikali imekuja na mpango wa Bima ya CHF ili kuwarahisishia kuhusu hilo.

“ Nafahamu wazee wengine hapa mnaishi na wajuukuu zenu kwaiyo wanapougua mnalazimika kuingia gharama nyingine za matibabu,niwaambie tu sasa hivi kuna CHF ambayo mnaweza kutibiwa hadi watu sita kwa shilingi elfu thelathini tu kwa mwaka mzima,hii itasaidia wazee msipate usumbufu wa kuingia gharama za ziada wakati wewe unatibiwa bure”Alisema

Vilevile Dkt Lutalala ameeleza kuwa ili kujiandikisha mwananchi anapaswa kwenda katika Ofisi ya kijiji ambako kuna waandikishaji walioteuliwa na Serikali ya Kijiji na kuwa hivi sasa kwa mwenye kadi hiyo anaweza kupata matibabu ndani ya Mikoa yote ya Tanzania Bara

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *