Mkenya Peres aweka rekodi katika mbio za nusu marathon, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 5, 2020

Mwanariadha wa Kenya Peres Jepchirchir ameweka rekodi ya dunia katika mashindano ya mbio za nusu marathon kwa wanawake kwa kutumia saa 1, dakika 5 na sekunde 34. Jepchirchir mwenye umri wa miaka 26 ameibuka na ushindi huo katika mchuano uliofanyika Asubuhi ya leo katika uwanja wa Letna Park katika mji mkuu wa jamhuri ya Czech, Prague. Rekodi ya awali ambayo ilikuwa ya saa 1, dakika 6 na sekunde 11, iliwekwa mwaka 2018 na Netsanet Gudet wa Ethiopia. Rekodi hiyo iliwekwa katika mchuano wa kutafuta bingwa wa nusu marathoni uliofanyika Valencia, Uhispania.,

Mwanariadha wa Kenya Peres Jepchirchir ameweka rekodi ya dunia katika mashindano ya mbio za nusu marathon kwa wanawake kwa kutumia saa 1, dakika 5 na sekunde 34. 

Jepchirchir mwenye umri wa miaka 26 ameibuka na ushindi huo katika mchuano uliofanyika Asubuhi ya leo katika uwanja wa Letna Park katika mji mkuu wa jamhuri ya Czech, Prague.

 Rekodi ya awali ambayo ilikuwa ya saa 1, dakika 6 na sekunde 11, iliwekwa mwaka 2018 na Netsanet Gudet wa Ethiopia. Rekodi hiyo iliwekwa katika mchuano wa kutafuta bingwa wa nusu marathoni uliofanyika Valencia, Uhispania.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *