Mkenge akumbana na kilio cha barabara Kerege, on September 10, 2020 at 3:00 pm

September 10, 2020

Na Omary Mngindo, KeregeMGOMBEA Ubunge Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharami Mkenge amepokelewa na adha ya barabara inayowakabili wakazi waishio vitongoji ndani ya Kata ya Kerege.Sanjali na barabara pia amepokea kilio cha kukosekana kwa shule ya msingi katika Kitongoji cha Amani, ambapo imeelezwa kwamba wanafunzi wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata masomo.Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katani hapo Athumani Kaluma, akiongea kabla ya mgombea huyo kuzungumza na wananchi, ambapo alisema baadhi ya vitongoji vina changamoto ya barabara, hivyo pindi atakapochaguliwa azifanyiekazi kero hizo.”Utakapochaguliwa utuangalie wakazi wa Kata ya Kerege, tunachangamoto kubwa ya barabara maeneo yetu mengi hayapitiki kutokana na miundombinu yake kuharibika vibaya, pia kitongoji cha Amani hakuna shule hivyo vijana wetu wanatembea umbali mrefu kufuata shule,” alisema Kaluma.Akizungumza na wakazi hao, Mkenge alianza kumshukuru Mwenyekiti huyo, huku akieleza kuwa chabgamoto za barabara na shule anazitambua, ambapo alisema kuwa pindi wana-Bagamoyo wakikipatia ridhaa chama hicho watahakikisha wanakabiliana na adha hiyo.”Adha ya miundombinu ya baadhi ya barabara katika Vitongoji vinavyounda Kata ya Kerege nazifahamu, kwani mara kadhaa nilikiwa napita buneziona kero hizo, niwaombe wana-Kerege siku ya Oktoba 28 tujitokeze kwa wingi kumpigia kura mgombea wetu wa Urais Dkt. John Magufuli, Mimi Mbunge na Diwani Said Ngatipula,” alisema Mkenge.Aidha aliongeza kuwa yeye ni mmoja wa wapenda maendeleo wa jimbo la Bagamoyo, kwa kusimamia ujenzi wa Kampuni ya Bagamoyo Sugar ambao kwa sasa ujenzi wake unaendelea vizuri.Wakati Rais wetu Dkt. John Magufuli alipoirejesha ardhi ekta elfu kumi mikononi mwa serikali, alikutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Azam chini ya Mkurugenzi Said Bahkresa ili apatiwe ardhi hiyo kwa ajili ya kilimo cha miwa.”Baada ya kuzungumza na Mheshimiwa Rais, Mkurugenzi Bahkresa aliniita akaniambia suala hilo nami nikaanza kufuatilia suala hilo, mpaka sasa kilimo cha miwa kinaendelea na ujenzi wake upo ukingoni,” alisema Mkenge.Alisema kuwa katika kipindi hiki kuna wana-Bagamoyo wanaofanyakazi huku akiongeza kuwa mpaka kitakapokamilika kinataraji kuajili wananchi zaidi ya elfumoja.Awali ameneja wa Kampeni Yahya Msonde aliwataka wana-Bagamoyo kutopepesa macho Oktoba 28, badala yake wapigekura za kutosha kwa wagombea wote wanaotokea chama hicho, haswa kura za kishindo kwa mgombea urais Dkt. John Magufuli.,

Na Omary Mngindo, Kerege
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharami Mkenge amepokelewa na adha ya barabara inayowakabili wakazi waishio vitongoji ndani ya Kata ya Kerege.

Sanjali na barabara pia amepokea kilio cha kukosekana kwa shule ya msingi katika Kitongoji cha Amani, ambapo imeelezwa kwamba wanafunzi wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata masomo.

Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katani hapo Athumani Kaluma, akiongea kabla ya mgombea huyo kuzungumza na wananchi, ambapo alisema baadhi ya vitongoji vina changamoto ya barabara, hivyo pindi atakapochaguliwa azifanyiekazi kero hizo.

“Utakapochaguliwa utuangalie wakazi wa Kata ya Kerege, tunachangamoto kubwa ya barabara maeneo yetu mengi hayapitiki kutokana na miundombinu yake kuharibika vibaya, pia kitongoji cha Amani hakuna shule hivyo vijana wetu wanatembea umbali mrefu kufuata shule,” alisema Kaluma.

Akizungumza na wakazi hao, Mkenge alianza kumshukuru Mwenyekiti huyo, huku akieleza kuwa chabgamoto za barabara na shule anazitambua, ambapo alisema kuwa pindi wana-Bagamoyo wakikipatia ridhaa chama hicho watahakikisha wanakabiliana na adha hiyo.

“Adha ya miundombinu ya baadhi ya barabara katika Vitongoji vinavyounda Kata ya Kerege nazifahamu, kwani mara kadhaa nilikiwa napita buneziona kero hizo, niwaombe wana-Kerege siku ya Oktoba 28 tujitokeze kwa wingi kumpigia kura mgombea wetu wa Urais Dkt. John Magufuli, Mimi Mbunge na Diwani Said Ngatipula,” alisema Mkenge.

Aidha aliongeza kuwa yeye ni mmoja wa wapenda maendeleo wa jimbo la Bagamoyo, kwa kusimamia ujenzi wa Kampuni ya Bagamoyo Sugar ambao kwa sasa ujenzi wake unaendelea vizuri.

Wakati Rais wetu Dkt. John Magufuli alipoirejesha ardhi ekta elfu kumi mikononi mwa serikali, alikutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Azam chini ya Mkurugenzi Said Bahkresa ili apatiwe ardhi hiyo kwa ajili ya kilimo cha miwa.

“Baada ya kuzungumza na Mheshimiwa Rais, Mkurugenzi Bahkresa aliniita akaniambia suala hilo nami nikaanza kufuatilia suala hilo, mpaka sasa kilimo cha miwa kinaendelea na ujenzi wake upo ukingoni,” alisema Mkenge.

Alisema kuwa katika kipindi hiki kuna wana-Bagamoyo wanaofanyakazi huku akiongeza kuwa mpaka kitakapokamilika kinataraji kuajili wananchi zaidi ya elfumoja.

Awali ameneja wa Kampeni Yahya Msonde aliwataka wana-Bagamoyo kutopepesa macho Oktoba 28, badala yake wapigekura za kutosha kwa wagombea wote wanaotokea chama hicho, haswa kura za kishindo kwa mgombea urais Dkt. John Magufuli.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *