Mke Wa Carlinhos Adatishwa Na Mashabiki Yanga

September 15, 2020

MREMBO  Vanessa ambaye ni mke wa kiungo mpya wa Yanga, Carlinhos, raia wa Angola, amekuwa akionyesha mahaba yake waziwazi kwa staa huyo kwenye mitandao ya kijamii.Lakini juzi alionekana kukunwa na mashabiki wa Yanga kwa jinsi walivyompokea mumewe wakati akitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea kwao Angola.Vanessa alitupia video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikionyesha jinsi Carlinhos alivyopokewa kwa shangwe na mashabiki wa Yanga, kisha akaandika maneno haya:“Mpenzi wangu…tumshukuru Mungu kwa namna gani? Kwa baraka hiyo, nina furaha hukuacha kujiamini hata kila mmoja alipokoma kukuamini.Ni Mungu pekee ndiye anayejua nyakati za usiku tulizotumia kwenye maombi.“Siku zote nilikuambia wakati wako utafika, kipaji, unyenyekevu siku zote zinaendelea kuwa nawe. Ni Baba tu wa mbinguni anayeweza kufanya hayo.Tunafurahi kujua kwamba umepokewa vizuri katika namna hii kwenye nchi ambayo haijulikani kabisa kwetu.“Mungu aendelee kuwa pamoja nawe, atembee nawe, usimsahau Mungu mpenzi…nakutakia mafanikio endelevu katika hatua hiyo mpya. Fanya kile unachojua kukifanya kwa ubora; KUCHEZA MPIRA.” Wapendanao hao wawili wana watoto watatu.,

MREMBO  Vanessa ambaye ni mke wa kiungo mpya wa Yanga, Carlinhos, raia wa Angola, amekuwa akionyesha mahaba yake waziwazi kwa staa huyo kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini juzi alionekana kukunwa na mashabiki wa Yanga kwa jinsi walivyompokea mumewe wakati akitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea kwao Angola.

Vanessa alitupia video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikionyesha jinsi Carlinhos alivyopokewa kwa shangwe na mashabiki wa Yanga, kisha akaandika maneno haya:“Mpenzi wangu…tumshukuru Mungu kwa namna gani? Kwa baraka hiyo, nina furaha hukuacha kujiamini hata kila mmoja alipokoma kukuamini.

Ni Mungu pekee ndiye anayejua nyakati za usiku tulizotumia kwenye maombi.

“Siku zote nilikuambia wakati wako utafika, kipaji, unyenyekevu siku zote zinaendelea kuwa nawe. Ni Baba tu wa mbinguni anayeweza kufanya hayo.

Tunafurahi kujua kwamba umepokewa vizuri katika namna hii kwenye nchi ambayo haijulikani kabisa kwetu.“Mungu aendelee kuwa pamoja nawe, atembee nawe, usimsahau Mungu mpenzi…nakutakia mafanikio endelevu katika hatua hiyo mpya. Fanya kile unachojua kukifanya kwa ubora; KUCHEZA MPIRA.” Wapendanao hao wawili wana watoto watatu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *