Mkasa Mzima wa Mvuvi Aliyevua Samaki Albino Huu Hapa….

October 6, 2020

 

Mvuvi Jason Gillespie kutokea nchini Uingereza, amesema amepata bahati ya kuvua samaki aina ya papa mwenye ‘Albinism’  ambapo akapiga naye picha kisha kumrudisha tena baharini.

Kwa mujibu wa TMZ, Jason Gillespie amesema alikuwa anavua samaki na marafiki zake karibia na maeneo ya ‘Isle of Wight’ ndipo alipomvua papa huyo mwenye ‘albinism’ ya rangi nyeupe tupu ambaye alikuwa na futi 3.

“Nimekuwa nafanya kazi ya uvuvi kwa kipindi cha miaka 30 kamwe sikuwahi kuona mmoja kama huyu, nilimuachia kwa sababu ni spishi inayolindwa, nilijua ilikuwa kitu maalum kwa hiyo nikapiga naye picha kisha nikamuachia baharini, ilikuwa ni nafasi kwangu sijui niseme nini, ni samaki wa maisha moja kati ya milioni” amesema Jason Gillspie 

Inaaminika Jason Gillespie ndiye mvuvi pekee aliyepata udhibitisho wa papa mwenye albinism japo mwenyewe amesema aliwahi kusikia mvuvi mwingine kutoka Wales alivua papa kama huyo mwaka mmoja uliopita ila alikuwa mdogo sana.

Papa hao wenye ‘albinism’ huishi tofauti na papa wengine kutokana na rangi zao, pia huwa hawaonekani kwa sababu wanajificha sana wakati wa uvuvi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *