Miquissone na Wawa kutoivaa Namungo Kesho?, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 29, 2020 at 4:38 pm

August 29, 2020

Klabu ya soka ya Simba itawakosa nyota wake Luis Miquissone na mlinzi Pascal Wawa katika mchezo wa kesho dhidi ya Namungo ambao ni wa ngao ya jamii ikiwa ni kiashirio cha ufunguzi wa pazia wa igi kuu ya Tanzania Bara.Akizungumza na Waandishi wa Habari ,Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandebroeck amesema kukosekana kwa nyoa hao ni kutokana na kukosa utimamu wa mwili kwa kuwa walisafiri nje ya nchi kwa masuala ya kifamilia hivyo hawakushiriki mazoezi na wenzao wakati wa maandalizi.Katika hatua nyingine kocha huyo raia wa Ubelgiji amelalamikia maandalizi ya Uwanja ambao hawajapata nafasi ya kufanyia mazoezi,ingawa amesema Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linafanya kazi nzuri ya kuupeleka mpira maeneo mbalimbali lakini alishauri kuzingatiwa kwa maandalizi bora .Vilevile Sven amesema mchezo wa kesho dhidi ya Namungo utakua wa tofauti kwa kuwa Timu zina maingizo mapya ya wachezaji na hawakupata muda mrefu wa maandalizi .Kwa upande wa Kocha wa Namungo, Hitimana Thiery ameonyesha wasiwasi kuelekea mcheo huo kutokana na Timu yake kuwa na wachezaji wengi wapya ambao pia yeye hakushiriki moja kwa moja katika usajili wao.REKODI ZINAZOWEZA KUWEKWAIwapo Simba itashinda taji la Ngao ya Jamii,itaweka rekodi ya kuwa Timu iliyotwaa mara nyingi zaidi yaani mara 6 na kuipiku Yanga ambayo imetwaa mara tano.,

Klabu ya soka ya Simba itawakosa nyota wake Luis Miquissone na mlinzi Pascal Wawa katika mchezo wa kesho dhidi ya Namungo ambao ni wa ngao ya jamii ikiwa ni kiashirio cha ufunguzi wa pazia wa igi kuu ya Tanzania Bara.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ,Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandebroeck amesema kukosekana kwa nyoa hao ni kutokana na kukosa utimamu wa mwili kwa kuwa walisafiri nje ya nchi kwa masuala ya kifamilia hivyo hawakushiriki mazoezi na wenzao wakati wa maandalizi.

Katika hatua nyingine kocha huyo raia wa Ubelgiji amelalamikia maandalizi ya Uwanja ambao hawajapata nafasi ya kufanyia mazoezi,ingawa amesema Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linafanya kazi nzuri ya kuupeleka mpira maeneo mbalimbali lakini alishauri kuzingatiwa kwa maandalizi bora .

Vilevile Sven amesema mchezo wa kesho dhidi ya Namungo utakua wa tofauti kwa kuwa Timu zina maingizo mapya ya wachezaji na hawakupata muda mrefu wa maandalizi .

Kwa upande wa Kocha wa Namungo, Hitimana Thiery ameonyesha wasiwasi kuelekea mcheo huo kutokana na Timu yake kuwa na wachezaji wengi wapya ambao pia yeye hakushiriki moja kwa moja katika usajili wao.

REKODI ZINAZOWEZA KUWEKWA

Iwapo Simba itashinda taji la Ngao ya Jamii,itaweka rekodi ya kuwa Timu iliyotwaa mara nyingi zaidi yaani mara 6 na kuipiku Yanga ambayo imetwaa mara tano.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *