Microsoft: Wadukuzi wa mtandao wa Urusi, China na Iran walenga taarifa za Trump na Biden, on September 11, 2020 at 8:00 am

September 11, 2020

 Wadukuzi wenye uhusiano na Urusi China na Iran wanajaribu kuingilia taarifa za watu na makundi yanayohusika na uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2020 , Microsoft imesema.Wadukuzi wa Urusi ambao waliweza kuingilia kampeni za mwaka 2016 za chama cha Democratic kwa mara nyingine tena wamehusika katika udukuzi wa sasa, imesema kampuni hiyo ya teknolojia.Microsoft imesema ilikuwa “wazi kwamba shughuli za makundi ya kigeni yalifanya juhudi zao ” kuulenga uchaguzi.Kampeni ya Donald Trump na hasimu wake upande wa Democratic Joe Biden zinalengwa katika tovuti za mashambulio ya kimtandao .Wadukuzi kutoka kikundi cha Strotium wamelenga zaidi ya makampuni 200 ambayo mengi kati yake yana uhusiano na vyama vya kisiasa vya Marekani-vyote cha Warepublicans na Wademocrats, imesema taarifa ya Microsoft.Washambuliaji wa kimtandao pia walilenga vyama vya kisiasa vya Uingereza, imesema Microsoft, bila kuvitaja ni vipi.Strontium pia kinafahamika kama Fancy Bear, kitengo cha mashambulio ya kimtandao kinachodaiwa kuwa na uhusiano na idara ya ujasusi ya jeshi la Urusi, GRU.,

 

Wadukuzi wenye uhusiano na Urusi China na Iran wanajaribu kuingilia taarifa za watu na makundi yanayohusika na uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2020 , Microsoft imesema.

Wadukuzi wa Urusi ambao waliweza kuingilia kampeni za mwaka 2016 za chama cha Democratic kwa mara nyingine tena wamehusika katika udukuzi wa sasa, imesema kampuni hiyo ya teknolojia.

Microsoft imesema ilikuwa “wazi kwamba shughuli za makundi ya kigeni yalifanya juhudi zao ” kuulenga uchaguzi.

Kampeni ya Donald Trump na hasimu wake upande wa Democratic Joe Biden zinalengwa katika tovuti za mashambulio ya kimtandao .

Wadukuzi kutoka kikundi cha Strotium wamelenga zaidi ya makampuni 200 ambayo mengi kati yake yana uhusiano na vyama vya kisiasa vya Marekani-vyote cha Warepublicans na Wademocrats, imesema taarifa ya Microsoft.

Washambuliaji wa kimtandao pia walilenga vyama vya kisiasa vya Uingereza, imesema Microsoft, bila kuvitaja ni vipi.

Strontium pia kinafahamika kama Fancy Bear, kitengo cha mashambulio ya kimtandao kinachodaiwa kuwa na uhusiano na idara ya ujasusi ya jeshi la Urusi, GRU.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *